Habari za Punde

Maalim Seif ashiriki Mazishi ya Hemed Salum Hemed

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akishiriki katika mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) mkaazi wa Kinuni Zanzibar aliyefariki katika ajali ya barabarani wakati akitoka mkutanoni Makunduchi. Mazishi hayo yamefanyika Msikiti Ngamia, Kilimahewa.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akishiriki katika mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) mkaazi wa Kinuni Zanzibar aliyefariki katika ajali ya barabarani wakati akitoka mkutanoni Makunduchi. Mazishi hayo yamefanyika Msikiti Ngamia, Kilimahewa.
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali mmoja kati ya watu waliojeruhiwa na watu wasiojulikana katika maeneo ya Fuoni Taveta, wakati wakirejea kutoka mkutano wa CUF Makunduchi. Amemtembelea kijana huyo Shamis Ali Khamis nyumbani kwao Muembe Makumbi mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).

Na: Khamis Haji (OMKR)

Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amehudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea wakati akirudi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

Marehemu ambaye ni mkaazi wa Kinuni, Wilaya ya Magharibi Unguja amesaliwa katika Msikiti Ngamia, Kilimahewa na kuzikwa Kianga, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Aidha, Maalim Seif amewatembelea na kuwawafariji baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliojeruhiwa na watu wasiojuilikana wakati walipokuwa wakirudi katika mkutano huo walipofika eneo la Fuoni.

Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa CUF bibi Pavu Juma, katika tukio hilo vijana waliokuwa katika gari eneo la Fuoni Taveta wakiwa na mapanga, nondo na mawe walianza kuwarushia mawe wafuasi wa CUF waliokuwa kwenye magari wakitokea katika mkutano Makunduchi na kuwajeruhi wafuasi 24 wa chama hicho

Amesema baadhi ya majeruhi hao wamepata majeraha makubwa na wamelazwa katika hospitali ya Mnazimmoja, na wengine wamesafirishwa hadi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Mapema akiwatembelea baadhi ya majeruhi huko Mwembemakumbi, Katibu Mkuu huyo wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema watu waliowajeruhi wafuasi wa CUF wamefanya hivyo baada ya chama chao kukosa Sera za kuwaeleza Wananchi na sasa wameamua kufanya hujuma ambazo amesema hazitowasaidia. 

Amerejea wito wake wa kuwataka wanachama na wafuasi wa CUF wawe watulivu na kwamba chama hicho kinafuatilia kwa karibu hujuma zote zinazofanywa dhidi yao.

1 comment:

  1. mnapoandika habari muwe wakweli mwogopeni mola ndugu zangu , kwa nini mnasema ajali wakati wameshambuliwa au mnajifanya kiswahili hamjui leo? ajli ya barabarani ni kugongwa au kugongana kwa vyombo kwa vyombo au chombo kugonga mtu , huyu aligongwa na gari ndugu mwandishi? usiwe mnafiki mola hawapendi wanafiki , najua hutochapisha haya maoni , muhimu wewe mwandishi wa hizi habari usipate ili umhabarishe huyu khamis haji aliyeandika hizi habari , ikifika ijumaa mstari wa mbele kuswali na masijida kama kovu kwenye vipaji , lakini unafiki umewatawala waandishi wa habari kwa kulinda matumbo yao , laana ya mola itakuwa juu yenu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.