Habari za Punde

Raza atoa msaada kwa wakristo jimboni kwake

  Raza akizungumza na Wakristu na wananchi wengine kabla ya kukabidhi chakula cha Pasaka kwa familia za Wakristu zenye maisha duni hapo Kiboje

Picha na Martin Kabemba

 Jacob Foda kwaniaba ya Wakristu wa dhehebu la Sabato akipokea vyakula kutoka kwa Mwakilishi wa Uzini Mohamed Raza huko Kiboje jana.
Picha na Martin Kabemba.
 Paulo John Ligema (kushoto) kwa niaba ya waumini wa kanisa la TAG akipokea vitabu vya Katiba iliyopendekezwa kutoka kwa Raza.
Picha na Martin Kabemba.

Mwakilishi wa jimbo la Uzini Zanzibar, Mohamed Raza amekabidhi mchele, unga wa ngano, mafuta, sukari na majani ya chai kwa familia zilizo duni za Wakristu wa madhehebu mbalimbali kwaajili ya  sikukuu ya Pasaka pamoja na vitabu vya Katiba iliyopendekezwa, kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki Kiboje jimbo la Uzini jana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.