Na
Ali Issa Maelezo-Zanzibar 17/4/2015
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa wananchi waliopewa nyumba za maendeleo za Serikali
na Rais wa kwanza wa Serikali ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume wataendelea
kuishi bure lakini watakapokufa wazee hao warithi wao watalazimika kulipa kodi
kama Serikali ilivyoagiza.
Hayo
yamesemwa leo katika ukumbi wa jengo la wasanii liliopo Rahaleo Mjini Zanzibar na
Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Abdalla Shaabani wakati
alipokuwa akizungumza na wakaazi wa nyumba hizo.
Amesema
kuwa watoto wa wamiliki wa nyumba hizo wataendelea kuishi humo bila ya
kubughudhiwa na mtu yoyote na jambo la muhimu ni kufuata agizo la Serikali juu
ya kuzitunza na kufuata sheria zilizowekwa ili nyumba hizo ziweze kudumu kwa
muda mrefu.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi tayari imeshapitisha maamuzi baada ya kukutana katika
vikao vyake na kuamua kuwa wakazi hao pamoja na wazee wao watakaa ndani ya nyumba
hizo bila kulipa kodi lakini kwa upande wa warithi watalazimika kulipa kodi
iliopangwa na Serikali ambayo itaaza rasmi ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.
“Uamuzi
wa Serikali kwa watu waliothibitika kupewa nyumba na Mzee Abeid Amani Karume
wataendelea kukaa bure, lakini mara tu watakapo kufa wazee hawa warithi wao
watalazimika kulipa kodi na huo ndio uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar” aliesma Waziri huyo.
Aidha
amewataka wananchi wanaokaa katika nyumba hizo kwenda kuchukua fomu za mikataba
kuanzia sasa na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuenzi juhudi za Mwanapinduzi
huyo na kuzilinda, kuzienzi na kuthamini mchangowake kwa Taifa la Zanzibar.
Nae
aliyekuwa Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume amesema kuwa Mzee Karume
katika uhai wake aliishi miaka saba tu baada ya Mapinduzi ambapo alijenga
nyumba za maendeleo na aliwapa watu wasiojiweza kimaisha kukaa nyumba hizo, lakini
leo hii kuna watu wanaojaribu kuwapotosha watoto wao kukaa humo bila ya malipo
ya kodi ameongeza kwa kusema kuwa kwa hivi sasa karibu ulimwengu mzima wananchi
wanakaa katika nyumba za serikali kwa kulipia kiwango kidogo cha kodi.
Nae
mmoja wa wakaazi wa nyumba hizo za
maendeleo Bi Zamzam amesikitikia kuwepo kwa kodi hiyo hivi sasa na kusema kuwa yeye
itamwiya vigumu kulipa kwani hali yake ni mzee, masikini, na hana kazi ya
kufanya, hivyo serikali iliangalie na hilo kwa watu wenye hali kama yake kwa
kuwasaidia juu sualazima la ulipaji.
Hongera waziri Shaaban na SMZ kwa ujumla kwa kuchukua maamuzi magumu na yanayotakiwa ktk Z'bar ya sasa.
ReplyDeleteVisiwa hivi vimebaki nyuma kwa mda mrefu kwa kukosa viongozi wenye maamzi ya namna hii.
Lazma tukubali kwamba maamuzi mema ya mzee KARUME baadhi ya watu wameyaelewa vibaya kwa mfano;
-Kuna watu wamepewa heka tatu-tatu lakini sasa wanazifanya za kwao wanarithishana, kugawana na kuziuza viwanja.
-Kuna waiopewa nyumba za kuishi kutokana na hali walizokua nazo, ndio hivyo tena...................
Pia kuna maamuzi ya jumla kama vile:
-Elimu bure kutokana na hali ya wakati ule lkn. cha kushangaza hadi leo hii mzee ukimwambia achangie 5000 tu kwa mwaka anakwambia KARUME alisema elimu bure.
-Kuna suala la maji ndio usiseme hoja ni zile zile au kubwa mtu atakwambia baadhi ya siku maji hayatoki!
-Matibabu ndio kabisa lkn.wakienda Bara au India ndio walipaji wazuri kabisa!
Naiomba serikali itupie jicho pia kwenye ntumba za WAKFU ili zikodishwe kwa bei ya soko ili zipatikane fedha za kutunza nyumba hizo na kuendelea kuwanufaisha wenyewe huko waliko
Nadhani wakati umefika wa kuchagua viongozi kama hawa wenye maamuzi sio tu " kana yawa kwetu!