Habari za Punde

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA)

Ofisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na Mratibu wa Mafunzo ya Waandishi wa Habari Haki za Binaadamu na Sheria za Waandishi wa Habari Zanzibar Bi Jina Mwinyi Waziri, akitowa maelezo kuhusiana na Huduma zinazotolewa na Kituo cha Sheria Zanzibar kwa waandishi wa habari wakati wa Semina hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Kituo hicho Migombani Zanzibar. 
Mwandhishi wa Habari Muandamizi Zanzibar Bi Maryam Hamdan akifungua Mafunzo ya Haki za Binaadamu na Sheria za SWaadishi wa Habari Zanzibar, mafunzo hayo yamewashirikisha waandishi Waandishi wa Habari mbalimbali Zanzibar, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAMAZA) yaliofanyika katika ukumbi wa kituo hicho migombani Zanzibar.kushoto Katibu Mtendaji wa Tume ya UtangazajiZanzibar Ndg Chande Omar na kulia Mwenyekiti wa WAHAMAZA Bi Salma Said
Washiriki wa Semina ya Waandishi wa Habari Zanzibar wakimsikiliza Bi Maryam Hamdan akitowa nasaha zake na Kuwataka waandishi kutumia Kalamu zao Vizuri wakati wa kuriopoti habari kwa wananchi.  
Waandishi wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa Semina hiyo, iliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Migombani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg Chande Omar akiwasilisha Mada ya Wajibu na Haki ya Kujua kwa Mwandishi wa Habari, wakati wa Semina ya Mafunzo ya Haki za Binaadamu na Sheria za Waandishi wa Habari, ilioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kushirikianda na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) iliowashirikisha waandishi wa habari wa Zanzibar iliofanyika katika kituo hicho migombani Zanzibar,  
Kamishna wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora , Mhe Mohammed Khamis akiwasilisha Mada ya Chimbuko la Historia na Maendeleo ya Haki za Binaadamu Kimataifa, Kikanda na Nchini Tanzania, wakati wa mafunzo ya semina kwa waandishi wa habari Zanzibar kujua na kuelewa Haki za Binaadamu. semina hiyo  imefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.

Mwandishi Mwandamizi Zanzibar Ndg Ali Saleh, akifafanua jambo kuhusiana na Sheria za Haki za Binaadamu wakati wa Semina hiyo ya Waandishi wa habari Zanzibar, ilioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, na kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) 
Meneja wa Baraza la Habari Tanzania Ndg Suleiman Seif, akiwakilisha Mada ya Habari za Mitandaoni na Maadili ya Waandishi wa Habari Zanzibar, wakati wa semina hiyo iliowashirikisha Waandishi wa habari Zanzibar kuelewa na wajibu wao katika uaandishi wa habari kwa jamii. 
Mwandishi wa Habari Muandamizi Zanzibar Ndg. Salim Said Salim akiwasilisha Mada yake Kanuni Miiko na Maadili ya Waandishi wa Habari Kimataifa na Kitaifa.wakati wa semina ya waandishi wa habari Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) Bi Salma Said akisisitiza jambo baada ya kuwasilishwa maada na kutowa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Migombani Zanzibar. 
             Waandishi wakiwa makini kufuatilima mafunzo hayo wakati ikiwakilishwa mada.
                      Mwandishi akichangia mada ilioowakilishwa katika semina hiyo.
Muandishi wa habari akichangia mada baada ya kuwakilishwa na muhusia wakati wa semina ya waandishi wa habari Zanzibar.
                       Mwandishi Talib akichangia wakati wa semina hiyo
                        Waandishi wakifuatilia michango iliowasilishwa na washiriki wa semina hiyo.
Waandishi wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmin Bi Maryam Hamdani, baada ya kuwafungulia semina yao katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Migombani Zanzibar,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.