UTANGULIZI:
1.0
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja kwamba Baraza lako Tukufu, likae kama
Kamati ya Mapato na Matumizi ili lipokee, lijadili na hatimae liidhinishe
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016.
2.0 Mheshimiwa
Spika, sina budi
kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuendelea kuijaalia nchi yetu amani na
utulivu na kutuwezesha kufanya kazi zetu kwa mafanikio. Vile vile nachukua nafasi hii kukushukuru wewe
Mheshimiwa Spika kwa kuliendesha Baraza letu kwa amani na salama na ufanisi
mkubwa.
3.0 Mheshimiwa
Spika, kwa aina ya kipekee
namshukuru na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa uongozi wake mahiri na usimamizi mzuri wa
shughuli za Serikali unaozingatia Katiba na Sheria za nchi. Mheshimiwa Rais amekuwa
mstahamilivu mkubwa, asiyetetereka na kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza
uwajibikaji na uadilifu katika utendaji wa shughuli za Serikali. Chini ya
uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, nchi
yetu imepiga hatua kubwa za maendeleo katika nyanja za kisiasa, kijamii na
kiuchumi. Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumpa kiongozi wetu huyu afya njema
na umri mrefu, yeye na familia yake na amzidishie hekima na busara ili aendelee
kuiongoza vyema nchi yetu.
4.0 Mheshimiwa Spika, aidha, namshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa
Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuendelea kumshauri vizuri na kumsaidia
Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi juu ya masuala
mbali mbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu. Pia namshukuru Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa
Rais kwa mashirikiano yake makubwa kwa Ofisi yangu.
5.0 Mheshimiwa Spika, Pia napenda kuwapongeza kwa dhati Naibu Spika, Mheshimiwa
Ali Abdalla Ali, Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini. Vile vile, nawashukuru
Wenyeviti wa Baraza, Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma, Mwakilishi wa Viti Maalum na
Mheshimiwa Mahmoud Mohamed Mussa, Mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni
kwa namna wanavyokusaidia katika kuliendesha Baraza letu hili.
6.0 Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii pia kuwashukuru Wenyeviti na
Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Baraza lako Tukufu kwa kusimamia vyema utendaji
katika Taasisi za Serikali ili kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yao kwa
ufanisi. Aidha, natoa shukrani maalum kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mheshimiwa Hamza Hassan Juma,
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Saleh Nassor
Juma, Mwakilishi wa Jimbo la Wawi na Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa kuyapitia
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ya mwaka
2015/2016 na kutupa ushauri utakaotuongoza katika utekelezaji wa malengo na
majukumu ya Ofisi yetu.
7.0 Mheshimiwa Spika, Pia nawapongeza Wajumbe wote wa Baraza hili Tukufu kwa
kuipitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016 iliyowasilishwa na Mheshimiwa
Waziri wa Fedha tarehe 13/05/2015. Bajeti hiyo ndiyo itakayoiwezesha Serikali
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa malengo iliyojiwekea katika shughuli za
kuwaletea maendeleo wananchi.
8.0 Mheshimiwa
Spika, kwa masikitiko
makubwa naomba nichukue fursa hii kumkumbuka ndugu yetu na mwenzetu Marehemu
Salmin Awadh Salmin alietutoka ghafla tarehe 19 Februari, 2015. Marehemu Salmin
alikua kiongozi shupavu, hodari na wakati wote alikuwa mstari wa mbele kutetea
wananchi na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu. Kuondoka kwake
kumeacha pengo kubwa na daima tutamkumbuka kwa mchango wake kwa jamii na nchi
yetu. Mungu ailaze roho ya Marehemu peponi, Amin. Aidha, natoa pole kwa wale wote waliopoteza
ndugu na jamaa zao katika maafa yaliyotokea tarehe 3 Mei, 2015 na waliopata
hasara ya kupotelewa na kuharibikiwa na mali zao. Serikali inachukuwa hatua
zinazostahiki kuona kwamba wale wote waliofikwa na maafa hayo wanarudi katika
hali ya maisha yao ya kawaida.
HALI YA
KISIASA:
9.0 Mheshimiwa
Spika, hali ya kisiasa
Zanzibar imeendelea kuwa ya shwari, amani na utulivu, hali ambayo imechangia
kwa kiasi kikubwa katika kuleta
maendeleo kwa kutoa fursa za uwekezaji, kufanyika kwa shughuli za biashara na
kutoa nafasi nzuri kwa wananchi kufanya
shughuli zao za kimaisha bila ya wasi
wasi. Hata hivyo, kunahitajika mashirikiano kwa Viongozi na wananchi wote ili
kuhakikisha amani na utulivu unazidi kuimarika katika nchi yetu, rasilimali
kubwa katika nchi yetu ni umoja, amani na utulivu, kwa hali yeyote lazima
tuilinde rasilimali hii.
10.0 Mheshimiwa Spika, mwaka huu nchi yetu inakabiliwa na mambo mawili makubwa na
muhimu, ambayo ni Kura ya Maoni kwa Katiba Inayopendekezwa ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania na Uchaguzi Mkuu. Kwa upande wa Kura ya Maoni, baada ya
kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa, wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa
ujumla watapata fursa ya kuipigia kura ya maoni Katiba hiyo katika tarehe
itakayotangazwa hapo baadae na Tume ya Uchaguzi. Napenda kuchukua nafasi hii
kwa mara nyengine tena kuwanasihi wananchi kuisoma na kuielewa Katiba hiyo ili
hatimae waweze kutoa maamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura. Kwa upande wake
Serikali imechukuwa juhudi ya kugawa nakala za Katiba Inayopendekezwa kwa
wananchi Unguja na Pemba. Ni imani yangu kuwa wananchi wote wenye sifa za
kupiga kura wataitumia fursa hii adhimu ya kuitumia haki yao ya kidemokrasia
kwa kwenda kupiga kura ya maoni.
11.0 Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa
Uchaguzi Mkuu, wananchi watapata fursa ya kuchagua viongozi wao wakiwemo Rais
wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi, Wabunge, na Madiwani ambao watawatumikia katika kipindi cha miaka
mitano ijayo. Katika kufanikisha zoezi hilo, nawaomba wananchi ambao bado
hawajajiandikisha na wanazo sifa za kufanya hivyo waende kujiandikisha katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura
muda utakapowadia.
12.0 Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa
maandalizi ya uchaguzi huo, Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar inaendelea vyema na matayarisho ikiwemo uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kutoa Elimu ya Wapiga Kura na upatikanaji wa
vifaa mbali mbali vya upigaji kura. Serikali kwa upande wake itahakikisha
kwamba, Uchaguzi Mkuu huo utakuwa wa haki na utafanyika katika hali ya utulivu,
usalama na amani. Hivyo tunaomba wanasiasa wote wasiwe chanzo cha kuharibu
amani na upendo uliopo bali wawe chanzo cha kuimairisha amani, umoja na upendo.
HALI YA
UCHUMI WA ZANZIBAR:
13.0 Mheshimiwa
Spika, kama alivyoeleza
Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora wakati
akiwasilisha hali ya uchumi kwa mwaka 2014 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka
2015/2016 katika Baraza lako Tukufu, uchumi wa Zanzibar kwa kipindi cha miaka
mitano kuanzia mwaka 2010/2014 umeonesha mwenendo mzuri na umekua kwa kiwango
cha kuridhisha cha wastani wa asilimia 6.5. Ukuaji huo wa uchumi ulitokana na
kuimarika kwa sekta ndogo za Ujenzi, Fedha na Bima, Usafiri, Habari na
Mawasiliano na Sekta ndogo ya Utawala wa Umma.
14.0 Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Pato la Taifa kwa mwaka 2014, Pato halisi lilikua kwa
kiwango cha wastani wa asilimia 7.0 ikilinganishwa na wastani wa 7.2 mwaka
2013. Kuongezeka kwa pato la Taifa kumechangiwa na mambo makuu yafuatayo:-
i.
Kuimarika kwa sekta ya huduma ambayo imekuwa
kutoka asilimia 4.6 mwaka 2013 hadi asilimia 9.8 mwaka 2014.
ii.
Kuimarika
kwa sekta ya viwanda ambayo imekuwa kutoka asilimia 3.5 mwaka 2013 hadi
asilimia 6.0 mwaka 2014.
iii.
Kuongezeka
kwa idadi ya watalii walioingia nchini kutoka watalii 181,301 mwaka 2013 hadi
kufikia watalii 311,891 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 72.
iv.
Kuwepo
kwa hali ya amani na utulivu nchini.
15.0 Mheshimiwa
Spika, kuendelea kukuwa
kwa uchumi wa Zanzibar kunatokana na juhudi za Serikali za kukuza uchumi kwa
kutekeleza mipango, mikakati na sera mbalimbali za kiuchumi. Juhudi ambazo
zitaendelezwa ili kuimarisha hali ya ustawi wa wananchi wa Zanzibar. Kama
ilivyokwisha elezwa na Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa mwaka ujao maeneo muhimu
yatakayopewa kipaumbele na Serikali ni miundombinu na mawasiliano, huduma za kielimu, afya, na pensheni kwa
wazee waliofikia miaka 70 na zaidi.
HUDUMA ZA
JAMII:
16.0 Mheshimiwa
Spika, katika Awamu hii ya
Saba, Serikali imechukua hatua mbali mbali za kuimarisha huduma za elimu, afya,
maji safi na salama pamoja na makaazi ili kuleta ustawi mzuri kwa jamii. Kwa
upande wa Sekta ya Elimu, Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za
kuiimarisha na kuiendeleza elimu. Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa skuli na
madarasa mapya kwa skuli za Maandalizi, Msingi na Sekondari, ununuzi wa samani
pamoja na vitabu vya kiada, ziada na vya maktaba kwa skuli mbali mbali za
Unguja na Pemba. Aidha, Serikali
imeendelea kuwajengea uwezo walimu kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi
kwa lengo la kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa.
17.0 Mheshimiwa Spika, hivi karibuni Serikali imetangaza rasmi kufuta michango
yote iliyokuwa ikitolewa na wananchi kwa ajili ya elimu ya msingi ya watoto wao
na kuondosha ada za mitihani kwa elimu ya sekondari. Uamuzi huu wa Serikali una
lengo la kuwaondoshea wananchi hasa wa kipato cha chini mzigo wa kugharamia
elimu ya watoto wao na kutoa fursa zaidi kwa watoto wetu kupata elimu na
kujenga Taifa la watu walioelimika. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa uamuzi huu
wa Serikali yake ambao unawajali sana wananchi.
18.0 Mheshimiwa
Spika, Serikali inaendelea
kuweka mazingira mazuri ya kuwawezesha wanafunzi kujiunga na kuendelea na
masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbali mbali ndani na nje ya nchi kwa
kuwapatia mikopo wale wote wanaokidhi vigezo vya kupatiwa mikopo hiyo. Serikali
itaendelea kutoa huduma hii ya mikopo ya elimu ya juu ili kufikia lengo la kuwa
na wataalamu wazalendo katika fani mbali mbali.
19.0 Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Sekta
ya Afya, Serikali imeendelea kuimarisha huduma za kinga na tiba katika
hospitali na vituo vya afya pamoja na kutoa elimu ya afya kwa wananchi ili
kujikinga na maradhi ya kuambukiza na yasio ya kuambukiza. Aidha, Serikali
imezifanyia matengenezo makubwa hospitali na vituo vya afya na kujenga majengo
mengine mapya Unguja na Pemba, ikiwemo wodi ya wagonjwa mahatuti (ICU) na
kitengo cha huduma ya upasuaji vichwa na uti wa mgongo (Neuro Surgical Unit)
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
20.0 Mheshimiwa
Spika, Serikali pia
imechukua hatua za kuongeza madaktari na wahudumu wengine wa afya kwa
kuwasomesha na kuwapatia uzoefu. Hivi sasa nchi yetu ina madaktari wazalendo
wapatao 44 na madaktari bingwa wazalendo 13. Hii ni hatua kubwa sana kufikiwa
na nchi yetu. Aidha, Serikali inawaendeleza madaktari 14 kuwa madaktari bingwa
wa saratani, maradhi ya watoto, maradhi ya kina mama, upasuaji wa uti wa
mgongo, maradhi ya mifupa na maradhi ya macho. Vile vile, kwa kushirikiana na
nchi marafiki, Serikali imepatiwa madaktari bingwa wa maradhi mbali mbali kwa
ajili ya kuwahudumia wananchi wetu.
21.0 Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Sekta
ya Maji, Serikali imeendelea na juhudi zake za kuwapatia wananchi huduma bora
ya maji safi na salama. Katika kutimiza lengo hilo, Serikali inaendelea
kutekeleza programu na miradi mbali mbali ikiwemo uchimbaji wa visima, ujenzi
wa matangi ya maji na uwekaji wa pampu na mota. Pia kufanya matengenezo makubwa
katika miundombinu ya usambazaji maji katika maeneo ya mijini na vijijini
Unguja na Pemba. Serikali itaendelea kuwaelimisha wananchi athari ya kuviharibu
na kuviziba vianzio vya maji ambavyo huweza kusababisha upungufu mkubwa wa
maji.
22.0 Mheshimiwa
Spika, Serikali kwa
kutambua umuhimu wa makaazi bora kwa wananchi wetu imeandaa Sheria ya Condominium ili kuwawezesha wananchi kumiliki sehemu ya majengo katika
nyumba za maendeleo na kuunda bodi ya kusimamia utekelezaji wa Sheria hiyo.
Aidha, Serikali imeandaa Sheria ya Shirika la Nyumba la Zanzibar ya mwaka 2014
ili kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba. Pia, Serikali inaufanyia
mapitio Mpango Mkuu wa Mji wa Zanzibar na kutenga maeneo maalum ya ujenzi wa
nyumba za ghorofa kwa lengo la kupunguza matumizi ya ardhi kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba.
MASUALA
MTAMBUKA:
Mazingira:
23.0 Mheshimiwa
Spika, utunzaji wa
mazingira ni suala muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. Nchi zote duniani
zinatoa kipaumbele katika suala hili kwa maendeleo endelevu na kupunguza
umasikini. Kwa kutambua umuhimu huo, Serikali imekua ikihimiza wananchi kupanda
miti kwa wingi na kuachana na tabia ya kukata miti ovyo na uchimbaji wa
rasilimali zisizorejesheka kiholela. Aidha, wananchi wanaelimishwa kuachana na
matumizi ya mifuko ya plastiki na kusafisha mazingira katika maeneo yao. Athari
ya mafuriko yanayoikumba nchi yetu mara kwa mara kwa kiasi kikubwa yanatokana
na uharibifu wa mazingira ikiwemo; uchimbaji wa mchanga kiholela, ujenzi wa
nyumba katika maeneo ya mabondeni, kwenye njia za maji ya mvua na utupaji wa
taka kiholela katika mitaro ya maji machafu.
Mapambano
Dhidi ya Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia:
24.0 Mheshimiwa
Spika, tatizo la ukatili
na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto bado linaendelea
kushamiri katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu licha ya jitihada kubwa
zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na tatizo hilo. Katika jitihada za
kuendelea na mapambano hayo, Serikali imeanzisha kamati za kupambana na ukatili
na udhalilishaji wa kijinsia katika ngazi ya taifa hadi shehia pamoja na
kuzijengea uwezo kamati hizo. Serikali pia inashirikiana na Asasi za Kiraia na
Viongozi wa Dini katika mapambano hayo. Kwa kutambua uzito wa tatizo hili, Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed
Shein mnamo tarehe 6 Disemba, 2014 alizindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya
‘’Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar Sasa Basi’’. Lengo la
Kampeni hii ni kuona kwamba hakuna tukio lolote la ukatili la udhalilishaji wa
wanawake na watoto litakalovumiliwa katika nchi yetu. Nachukua nafasi hii
kuwaomba viongozi na wananchi wote kuwafichua wanaofanya maovu haya na kuyapiga
vita kwa nguvu zetu zote.
Mapambano
dhidi ya Rushwa:
25.0 Mheshimiwa Spika, rushwa imekuwa donda ndugu na ni adui mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu na ustawi
wa jamii. Serikali inaendelea kuchukua hatua za kudhibiti vitendo vya kutoa na
kupokea rushwa kwa kuielimisha jamii kujua madhara ya rushwa na haja ya
kuichukia na kuikataa rushwa. Aidha, Serikali imetunga Sheria ya Kupambana na
Rushwa na Uhujumu Uchumi ya mwaka 2012 na kuanzisha Mamlaka ya Kupambana na
Rushwa na Uhujumu Uchumi. Serikali inaendelea kuijengea uwezo taasisi hii ili
iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
MALENGO NA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO KWA
KIPINDI CHA MIEZI TISA (JULAI-MACHI) 2014/2015
26.0 Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha
miezi tisa (Julai- Machi) cha mwaka wa fedha 2014/2015, Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais na Taasisi zake imechukua juhudi kubwa katika kutekeleza malengo
iliyojipangia na kufanikiwa kutekeleza yafuatayo:-
Ofisi ya
Faragha:
27.0 Mheshimiwa
Spika, Ofisi ya Faragha
kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
·
Kuimarisha
Ofisi ya Faragha ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais.
·
Kuimarisha
makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Plili wa Rais kwa kuzifanyia matengenezo nyumba
za Mazizini, Dar-es Salam na Dodoma.
·
Kuratibu
ziara 20 za ndani ya nchi na mbili (2) nje ya nchi za Mheshimiwa Makamu wa Pili
wa Rais.
·
Kuwajengea uwezo wafanyakazi wawili (2) wa Idara kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu
na muda mfupi pamoja na kulipia stahiki
za likizo kwa wafanyakazi wanne (4).
· Kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi na Taasisi mbali mbali za ndani, Kikanda na
Kimataifa.
Utekelezaji:
·
Ofisi ya Faragha imeratibu mikutano baina ya
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais na Mabalozi, Wanadiplomasia na Wageni mbali mbali
kutoka nchi za nje na Mashirika ya Kimataifa.
Mikutano hiyo imezidi kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Zanzibar na
nchi wanazotoka Wanadiplomasia na Wageni hao.
·
Ofisi imeratibu vikao vya mazungumzo ya upatanishi na utatuzi wa migogoro mbali mbali ya ardhi. Vikao hivyo vimefanikisha kumaliza
mgogoro wa wananchi wa Kiombamvua na Hotel ya Seacliff.
· Ofisi ya Faragha imeratibu ziara 33 za ndani za Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais. Ziara 29 zilihusisha Mikoa yote ya Zanzibar
na ziara nne (4) kwa Mikoa ya Tanzania Bara.
Madhumuni makuu ya ziara hizo yalikuwa ni kuonana na wananchi, kusikiliza
matatizo yao na kukagua shughuli zao za maendeleo. Aidha, Ofisi imeratibu ziara mbili (2) za nje
ya nchi, ziara hizo zilikuwa katika nchi za China na Zambia.
· Ofisi imeratibu ahadi 23
zilizotolewa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais katika mambo mbali mbali, kati
ya hizo ahadi tisa (9) tayari zimetekelezwa. Ahadi zilizokuwa hazijatekelezwa
zinaendelea kufanyiwa kazi na Taasisi mbali mbali zinazohusika.
28.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 483,116,224 kwa Ofisi ya Faragha. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla ya shilingi
449,644,209 zimepatikana na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa
na asilimia 93.
Idara ya
Uendeshaji na Utumishi:
29.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Uendeshaji
na Utumishi kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuweka mazingira mazuri ya kazi za Idara kwa
ununuzi wa vifaa vya ofisi, samani pamoja na kulipia gharama za umeme na
mawasiliano na utunzaji wa majengo.
• Kuufanyia mapitio Mpango wa Mafunzo ya
wafanyakazi pamoja kuandaa utaratibu wa kutathmini utendaji kazi (Staff
Appraisal System) na upandishaji vyeo wafanyakazi kwa kufuata Muundo wa
Utumishi (Scheme of Service).
• Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi.
• Kusimamia matumizi bora ya fedha na vifaa vya
ofisi kwa kuandaa vikao vinne (4) vya Kamati ya Uongozi, Vikao vinne (4) vya
Bodi ya Zabuni, vikao vinne vya Kamati ya Ukaguzi wa Ndani na kulifanyia
mapitio Daftari la Mali za Serikali (Asset Registry).
Utekelezaji:
• Jumla ya wafanyakazi 38 wamepatiwa mafunzo
ya muda mrefu na muda mfupi katika fani mbali mbali ndani na nje ya nchi ili
kuwaongezea ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
zaidi.
• Idara imenunua vifaa na vitendea kazi mbali mbali kwa matumizi ya ofisi pamoja na
kulipia gharama za uendeshaji wa ofisi kama vile maji, umeme na mawasiliano ya
simu na intaneti.
• Idara imesimamia kwa mafanikio makubwa matumizi
bora ya fedha na rasilimali kwa kuandaa vikao vitatu (3) vya Kamati ya Uongozi,
Vikao vinne (4) vya Bodi ya Zabuni, vikao vitatu (3) vya Kamati ya Ukaguzi wa
Ndani na kulifanyia mapitio Daftari la Mali za Serikali (Asset Registry).
30.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 704,166,316 kwa Idara ya Uendeshaji na Utumishi. Hadi kufikia Machi,
2015 jumla ya Shilingi 584,539,975 zimepatikana
na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa na asilimia 83.
Idara ya
Mipango, Sera na Utafiti:
31.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Mipango,
Sera na Utafiti kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuratibu vikao 12 vya Kamati ya Kisekta ya kuidhinisha Tafiti mbali mbali na
Vikao vinne (4) vya Kamati ya Taifa ya Kutafiti Rasilimali za Asili.
• Kuratibu utekelezaji wa Miradi ya Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na
Malaria kupitia Mfuko wa Dunia (Global Fund).
• Kuandaa Bajeti na kutayarisha Miradi ya
Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2015/2016
na kufanya ziara nne (4) za ufuatiliaji wa utekelezaji wa Programu/ Miradi ya
Maendeleo.
• Kufanya
mapitio ya Mpango Mkakati (SP) 2012-2014
wa Ofisi Makamu wa Pili wa Rais.
• Kuwajengea uwezo wafanyakazi 11 wa Idara
kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na wafanyakazi watatu (3) muda mrefu na
kulipa stahiki za likizo za wafanyakazi watatu (3).
• Kwa kushirikiana na COSTECH kuwajengea uwezo watafiti wa Wizara za SMZ kwa
kuandaa warsha mbili (2) pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa vibali
vya utafiti.
Utekelezaji:
• Idara imeandaa mafunzo ya Bajeti inayozingatia
Programu (PBB) yaliyowashirikisha Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi, Maafisa
Mipango na Wahasibu wa Ofisi/Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais.
• Idara imefanya vikao vitatu vya Kamati ya Utafiti ya kisekta, vikao hivyo
vilipokea na kupitisha maombi 10 ya utafiti.
• Idara ilifanya Semina huko
Pemba, semina hiyo ilihusu masuala ya utafiti na iliwashirikisha maofisa
utafiti, maafisa Mipango wa Wizara, wakuu wa vituo vya utafiti, NGO‘s
zinazojishughulisha na masuala ya utafiti na Vyuo vilivyopo Pemba.
• Idara imeandaa Taarifa za Utekelezaji kwa
kipindi cha miezi sita (6) Julai - Disemba na taarifa ya Utekelezaji miezi
mitatu (Oktoba – Disemba) pamoja na kutayarisha Mpango wa Matumizi wa Muda wa
Kati (MTEF) wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
• Idara imeufanyia mapitio Mpango Mkakati (SP)
wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
32.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 184,007,400 kwa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti. Hadi kufikia Machi,
2015 jumla ya Shilingi 134,207,903 zimepatikana
na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa na asilimia 73.
Idara ya
Uratibu wa Shughuli za Serikali:
33.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Uratibu wa
Shughuli za Serikali kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na
mfupi wafanyakazi wanne (4) pamoja na kulipia stahiki za likizo kwa wafanyakazi
saba (7).
• Kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuandaa Taarifa ya Utekelezaji kwa
kipindi cha miaka mitano, kuanzia Oktoba, 2010 – Mei, 2015.
• Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo
katika majimbo 50 ya Unguja na Pemba ambayo yamepatiwa fedha.
• Kusimamia utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Awamu ya
Tatu kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Unguja na Pemba.
• Kushughulikia malalamiko na migogoro ya wananchi kwa
kushirikiana na sekta husika.
• Kuratibu masuala ya Muungano.
• Kuimarisha Kitengo cha ICE kwa ununuzi wa vifaa
kutoa mafunzo kwa watendaji na kusimamia Tovuti ya Serikali.
• Kufuatilia mijadala na utekelezaji wa ahadi
za Serikali zinazotolewa katika vikao vya Baraza la Wawakilishi.
• Kuratibu vikao saba (7) vya mashirikiano na vikao vinne
(4) vya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa SMZ na SMT na vikao vinne (4) vya Sekreterieti
ya Kamati ya Pamoja ya Mambo ya Muungano.
Utekelezaji:
• Idara imeandaa Rasimu ya Taarifa ya
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
kwa kipindi cha miaka mitano (2010-2015).
• Idara imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa
Miradi midogo midogo ya wananchi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo katika Majimbo
32 ya Unguja na kukagua usahihi wa akaunti za mfuko huo katika Majimbo kumi
(10) kati ya 18 ya Pemba. Aidha, Idara imefuatilia marejesho ya matumizi ya
fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kwa mwaka 2013/2014. Kufuatia ufuatiliaji
huo, jumla ya Majimbo manane (8) yamefanya marejesho hadi kufikia Machi, 2015.
Majimbo hayo ni Donge, Kitope, Matemwe, Dimani, Makunduchi, Mtoni, Koani kwa
Unguja na Chambani kwa Pemba.
• Kuhusu masuala ya Muungano, Idara imeratibu
vikao vitano (5) vya mashirikiano baina ya Wizara za SMZ na SMT. Vikao hivyo
ni baina ya Kamati ya Wanasheria Wakuu
wa SMT na SMZ; Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati SMZ na Wizara ya
Nishati na Madini SMT; Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma SMZ na Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma SMT; Wizara ya Mifugo na Uvuvi SMZ na
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi SMT; na Wizara za Fedha za SMZ na SMT.
Aidha, Ofisi imeratibu vikao vinne (4) vya Sekretarieti ya mambo ya Muungano.
• Idara imesimamia utekelezaji wa Mpango wa
TASAF III wa Kunusuru Kaya Masikini. Mpango huo umefanikiwa kutekeleza kazi
zifuatazo:-
i.
Imefanikisha
zoezi la kuibua miradi ya kutoa ajira ya muda kwa kaya maskini na kuanza
utekelezaji wa miradi hiyo katika Shehia 40 za awali kwa Unguja na Pemba.
ii.
Imeandaa
mikutano kwa wajumbe 76 wa Kamati za Uongozi na Kamati za Usimamizi wa Mpango
wa TASAF III kwa Unguja na Pemba kwa lengo la kuwapatia uelewa wajumbe hao
kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini pamoja na taarifa za Mpango Kazi
zilizoandaliwa.
iii.
Usanifu
wa miradi ya kutoa ajira ya muda kwa kaya masikini umefanyika. Jumla ya miradi
77 (Unguja 33 na Pemba 44) imefanyiwa usanifu na imetekelezwa katika siku 60 za
mwaka wa kwanza. Miradi hiyo inahusiana na vitalu vya miti ya matunda na
misitu, upandaji wa miti ya mikoko, barabara za ndani, usafi wa mazingira na
ujenzi wa tuta la kuzuwia maji ya bahari. Jumla ya Shilingi 649,735,200 (Unguja
228,224,400 na Pemba 421,510,800) zimelipwa kwa kaya masikini 6,598 (Unguja
2,432 na Pemba 4,166) kwa miezi mitatu ya Disemba, Januari na Febuari. Aidha, kaya hizo masikini zimelipwa ruzuku ya
msingi na masharti ya jumla ya Shilingi 1,115,393,537 (Unguja 404,863,884 na
Pemba 710,529,653) katika kipindi cha miezi tisa (Julai-Machi).
iv. Uibuaji wa kaya
masikini katika Shehia 90 (Unguja 58 na Pemba 32) kwa ajili ya kufanyiwa
Tathmini ya Matokeo (Impact Evaluation) chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya
Masikini umefanyika. Tathmini hiyo inafanyika kwa mashirikiano baina ya Ofisi
ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali na TASAF Makao Makuu.
iv.
Uandikishaji
wa Kaya Masikini katika Shehia 51 mpya (Unguja Shehia 34 na Pemba Shehia 17)
umefanyika. Jumla ya Shehia 103 mpya (Unguja 68 na Pemba 35) zinatarajiwa
kuingizwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kuanzia mwaka huu wa 2015.
• Idara ya Uratibu, imekiimarisha Kitengo cha
Habari, Mawasiliano na Elimu (ICE) kwa kuwapatia mafunzo maafisa wanne wa
kitengo hicho na kupatiwa vifaa, ikiwemo kompyuta. Hili limefanyika kwa
mashirikiano na UNDP kupitia Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi za Viongozi
Wakuu wa SMZ.
• Idara imeendelea kuratibu utekelezaji wa ahadi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa
zilizotolewa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba wakati wa ziara
zilizofanywa na viongozi hao. Jumla ya ahadi 14 zimeratibiwa. Kati ya hizo,
ahadi nane (8) zimeshatekelezwa na sita (6) zinaendelea na hatua ya
kutekelezwa.
• Idara imeshughulikia jumla ya malalamiko 26
kwa kushirikiana na sekta husika. Malalamiko hayo yanahusiana na ardhi (15) na
mambo mengine (11).
34.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 344,638,000 kwa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali. Hadi kufikia
Machi, 2015 jumla ya Shilingi 231,909,954 zimepatikana na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa
na asilimia 67.
Idara ya
Uratibu Dar es Salaam:
35.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Uratibu
Dar es Salaam kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuweka mazingira mazuri ya kazi za Idara kwa
ununuzi wa vifaa vya ofisi na samani.
• Kuwapatia mafunzo wafanyakazi watatu (3) wa
Idara pamoja na kulipa stahiki za likizo
kwa wafanyakazi tisa (9).
• Kuandaa muundo mpya wa kitaasisi na
kiutumishi wa Idara utakaoleta ufanisi
na tija.
• Kuimarisha mashirikiano baina ya Idara na
Taasisi za SMZ na za SMT, Ofisi za
Kibalozi na Taasisi za Kimataifa
Utekelezaji:
• Idara imeshiriki mkutano wa wadau wa
uhamasishaji wa Mpango wa Utekelezaji
wa Viwanda vya Madawa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
• Idara imeshiriki katika kikao cha maandalizi
ya majadiliano baina ya Serikali ya Tanzania na Japan kuhusu ufadhili wa miradi
ya maendeleo kwa mwaka 2015/2016.
• Idara imeanza maandalizi ya kuandaa muundo
mpya wa Kitaasisi na Kiutumishi wa Idara.
• Idara imenunua vifaa vya kutendea kazi, kulipia huduma za ofisi (maji, umeme,
mawasiliano) na kulipia stahiki za likizo za wafanyakazi tisa (9).
36.0 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha
jumla ya Shilingi 353,178,160 kwa Idara ya Uratibu, Dar es Salaam. Hadi kufikia Machi,
2015 jumla ya Shilingi 181,504,731 zimepatikana
na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa na asilimia 51.
Idara ya
Kukabiliana na Maafa:
37.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Kukabiliana
na Maafa kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kujenga
uwezo kwa jamii katika kukabiliana na majanga na maafa kwa shehia 10.
• Kuyafanyia matengenezo maghala mawili (2) na
kununua vifaa vya kukabiliana na maafa Unguja na Pemba.
• Kukamilisha Sheria ya Kukabiliana na Maafa.
• Idara kwa Kushirikiana na Washirika wa
Maendeleo (USAFRICOM, Benki ya Dunia na
Kamisheni ya Bahari ya Hindi) itaendesha mafunzo mbali mbali ya kukabiliana na
maafa kwa watendaji na wadau pamoja na kuendesha mazoezi mawili (2) (Simulation
Exercise) ya kukabiliana na maafa.
• Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na
mfupi wafanyakazi wanne (4) na kulipa stahiki za likizo kwa wafanyakazi sita
(6).
Utekelezaji:
• Idara imeendesha zoezi la Kimataifa la
Kukabiliana na Maafa (Simulation
Exercise) lililoshirikisha wadau mbali mbali ambapo jumla ya watu 100 wameshiriki katika zoezi
hilo.
• Idara imejenga uwezo kwa jamii katika
kukabiliana na maafa na namna ya kupunguza athari zake kwa kutoa mafunzo kwa
Shehia 30 kwa Wilaya za Mjini, Magharibi, na Kaskazini “A” kwa Unguja na Wilaya
ya Chake Chake kwa Pemba. Aidha, Idara
imetoa elimu kupitia vipindi vya redio
katika Shirika la Utangazaji Zanzibar na
kuunda Kamati za Maafa kwa Shehia zilizopatiwa mafunzo.
• Idara imetoa mafunzo ya kujikinga na
Kukabiliana na Maafa kwa walimu 265 wa
Skuli za Serikali na Binafsi wa Wilaya za Mjini, Magharibi na Kaskazini ‘A’ kwa
Unguja na Wilaya ya Wete na Micheweni kwa Pemba.
• Idara imefanya tathmini na uchambuzi wa awali wa hali ya maafa kwa Shehia 30 katika
Wilaya za Kaskazini ‘B’ na Kati kwa Unguja na Wilaya za Chake Chake na Wete kwa
Pemba.
• Idara imeendesha semina ya siku moja ya Kujikinga na
kukabiliana na maafa kwa Viongozi 50 wa Vyama vya Siasa 22 vilivyosajiliwa.
• Idara imesambaza Kitabu cha Nyenzo za
Usimamiaji na Ufuatiliaji wa Sera ya
Kukabiliana na Maafa kwa wadau mbali mbali wa Maafa kwa Unguja na Pemba.
• Idara imezifanyia matengenezo makubwa ghala za kuhifadhia
vifaa vya Kukabiliana na Maafa Unguja na Pemba.
• Idara imesambaza Mkakati wa Ufuatiliaji Rasilimali
za Kukabiliana na Maafa kwa wadau mbali mbali wa Maafa Unguja na Pemba.
• Idara imefanya mkutano wa Kitaifa (Platform)
uliowashirikisha wadau mbali mbali wa maafa.
• Idara imekamilisha utayarishaji wa Sheria mpya ya Kukabiliana na Maafa.
38.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015
Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 298,447,800 kwa Idara ya Kukabiliana na Maafa. Hadi kufikia Machi,
2015 jumla ya Shilingi 196,518,500 zimepatikana
na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa na asilimia 66.
Idara ya
Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa:
39.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Sherehe na
Maadhimisho ya Kitaifa kwa mwaka 2014/2015 imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuratibu na kusimamia Sherehe za Miaka
51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
• Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na
mfupi wafanyakazi wawili pamoja na kulipa stahiki za likizo kwa wafanyakazi
wawili (2).
• Kuratibu Sherehe za Miaka 51 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ushiriki wa Viongozi na wananchi wa
Zanzibar katika Sherehe za Miaka 53 za Uhuru wa Tanganyika kwa kushirikiana na
Ofisi ya Waziri Mkuu.
• Kuifanyia mapitio Sheria namba 10 ya 2002 ya Kuwaenzi Viongozi pamoja na mambo
yanayohusiana nayo.
• Kuendelea kukusanya na kutunza kumbukumbu za Marehemu Sheikh Abeid Amani
Karume.
• Kuratibu Hitma na Dua ya Marehemu
Sheikh Abeid Amani Karume (Siku ya
Mashujaa).
Utekelezaji:
• Idara imeratibu Sherehe za Miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar kwa mafanikio makubwa. Aidha,
Ofisi imesimamia kilele cha sherehe hizo zilizofanyika tarehe 12 Januari, 2015,
Uwanja wa Amaan.
• Idara kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania imeanza maandalizi ya
kujenga kaburi la Marehemu Sheikh Idris Abdulwakil huko Makunduchi na kufanya
matengenezo ya kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume hapo Kisiwandui.
• Idara imeratibu maandalizi ya Sherehe za
miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar za tarehe 26 Aprili, 2015, Dar es Salaam.
• Idara imeratibu maandalizi ya maadhimisho ya
Siku ya Mashujaa Zanzibar (Karume Day) ya tarehe 7 Aprili, 2015.
40.0 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Baraza lako Tukufu
liliidhinisha jumla ya Shilingi 871,615,500 kwa Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa. Hadi
kufikia Machi, 2015 jumla ya Shilingi 1,358,989,917 zimepatikana na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa
na asilimia 156.
Idara ya
Upigaji Chapa na Mpiga chapa Mkuu wa Serikali:
41.0 Mheshimiwa
Spika, Idara ya Upigaji
Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, kwa mwaka 2014/2015 imepanga na
kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuweka mazingira mazuri ya kazi za Idara kwa
ununuzi wa vifaa vya ofisi na samani.
• Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na
mfupi wafanyakazi watano (5) na kulipa stahiki za likizo kwa wafanyakazi saba
(7).
• Kutoa huduma za Uchapishaji nyaraka na
Sheria za Serikali.
• Kutangaza huduma za Kiwanda kwa ajili ya kuongeza idadi ya wateja na mapato.
• Kukamilisha utaratibu wa kuanzisha Bohari kuu ya Serikali ya Vifaa vya Ofisi.
Utekelezaji:
• Idara imetayarisha Rasimu ya Sheria inayokipa
mamlaka Kiwanda cha Upigaji chapa iwe Taasisi inayojitegemea.
• Idara imenunua vitendea kazi na kulipia huduma za ofisi zikiwemo maji, umeme,
mawasiliano na kulipa stahiki za likizo kwa wafanyakazi saba (7).
• Idara kupitia Kiwanda cha Upigaji chapa
imefanikiwa kuchapisha nyaraka na
machapisho mbali mbali ya Serikali kama vile Gazeti Rasmi la Serikali, Miswaada
ya Sheria, Sheria na machapisho mengine yaliyowasilishwa kiwandani kwa mujibu
wa mahitaji ya Taasisi husika.
• Idara imeendelea na zoezi la kuzihamisha
Nyaraka zilizoko Saateni katika jengo la zamani la Kiwanda cha Uchapaji na kuzipeleka
Maruhubi. Nyaraka zote zimehifadhiwa vizuri na ziko salama.
42.0 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Baraza lako Tukufu
liliidhinisha jumla ya Shilingi 482,066,600 kwa Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla ya Shilingi 392,018,845 zimepatikana na kutumika kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa
na asilimia 81.
Baraza la
Wawakilishi:
43.0 Mheshimiwa
Spika, Baraza la
Wawakilishi kwa mwaka 2014/2015 limepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kujenga mazingira mazuri kwa kuwezesha kufanyika
kwa mikutano minne (4) ya Baraza la Wawakilishi pamoja na kazi za Kamati katika
kufuatilia shughuli za Serikali na kusimamia uwajibikaji wake.
• Kutoa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kitaalamu kwa Wajumbe
na wafanyakazi wa Baraza.
• Kutoa taaluma kwa wananchi kuhusu utendaji wa shughuli za Baraza kupitia Vyombo vya
Habari.
• Kuimarisha mahusiano kati ya Baraza na
Mabunge mengine ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola.
Utekelezaji:
• Baraza la Wawakilishi limefanya mikutano mitatu
ambayo ni mkutano wa 17, 18 na 19. Katika mikutano hiyo jumla ya Miswada 12
iliwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa. Jumla ya maswali ya misingi 169 na nyongeza
398 yaliulizwa na kujibiwa na waheshimiwa Mawaziri.
• Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi zilifanya kazi zake za kuisimamia Serikali na kufuatilia
utekelezaji wa shughuli za Serikali na kuwasilisha ripoti zao katika Mkutano wa
19 wa Baraza la Wawakilishi ambapo zilipokelewa na kujadiliwa. Aidha, Serikali
kupitia kila Wizara iliwasilisha ripoti za utekelezaji wa maagizo ya Kamati za
Baraza yaliyotokana na ripoti za Kamati za Kudumu za mwaka 2013/2014.
• Baraza lilipokea ripoti ya Kamati Teule ya Kuchunguza Upotevu wa Nyaraka za Serikali ambayo ilijadiliwa na Baraza kutoa
ushauri na maagizo kwa Serikali.
• Ofisi ya Baraza imefanya semina kwa asasi za kiraia, waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa
Baraza juu ya taratibu za ushirikishwaji wa wadau katika kazi za Kamati za
Baraza.
• Wanasheria saba (7) wa Baraza wamepatiwa
mafunzo ya siku tano (5) kuhusu
uandishi na kutafsiri sheria. Mafunzo hayo yalitolewa kupitia Taasisi ya Sheria
ya Kimataifa ya Uganda.
• Ofisi ya Baraza kwa kushirikiana na Shirika la Utangazji Zanzibar (Redio na TV)
linaendelea kurusha moja kwa moja (live) vikao vya Baraza la Wawakilishi.
Aidha, Baraza limekuwa likitoa taaluma kwa umma kupitia kipindi chake cha LIJUE
BARAZA LA WAWAKILISHI kipindi ambacho pia hurushwa kupitia Shirika hilo.
44.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 14,564,000,000 kwa Baraza la Wawakilishi. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla
ya Shilingi 13,954,901,100
zimepatikana na kutumika
kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa na asilimia 95.
Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar:
45.0 Mheshimiwa
Spika, Aidha, Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa mwaka 2014/2015
imepanga na kutekeleza yafuatayo:-
Malengo:
• Kuweka mazingira mazuri ya kazi za Tume kwa
ununuzi wa vifaa vya Ofisi na samani.
• Kuwajengea uwezo wafanyakazi watatu (3) kwa
kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na wafanyakazi 15 mafunzo ya muda mfupi pamoja
na kulipa stahiki za likizo kwa wafanyakazi sita.
• Kuendeleza Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
• Kufanya uchunguzi wa idadi, majina na mipaka
kwa Majimbo yote 50 ya Uchaguzi.
• Kusimamia na kuendesha Kura ya Maoni ya Kuthibitisha Katiba Inayopendekezwa.
• Kufanya matayarisho ya jumla ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015.
Utekelezaji:
• Tume ya Uchaguzi, imefanya matengenezo makubwa
ya Ofisi ya Wilaya ya Mjini kwa kuweka ukuta wa kizuizi na matengenezo ya
ukumbi wa mkutano. Kwa upande wa Pemba, Tume imefanya matengenezo makubwa ya
Ofisi ya Wilaya ya Wete pamoja na kununua vifaa na samani kwa ajili ya Ofisi
zote mbili.
• Tume ya Uchaguzi imefanya mapitio ya Kanuni, miongozo na maadili mbali mbali ya
uendeshaji na usimamizi wa shughuli za uchaguzi. Miongozo hiyo ni kama vile:
Maadili ya Vyama vya Siasa, Maadili ya Waangalizi wa Uchaguzi na Muongozo wa
Uteuzi kwa Wagombea.
• Tume ya Uchaguzi inaendelea na kazi za matayarisho ya
vielelezo vya kutoa elimu ya wapiga kura. Aidha, Tume imekamilisha muongozo kwa
ajili ya kutoa elimu ya Wapiga Kura kwa Asasi na Taasisi ambazo zinataka kutoa
elimu hiyo.
• Tume ya Uchaguzi inaendelea na maandalizi
ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Katika maandalizi hayo Tume ilikutana na Vyama
vya Siasa na wadau wa uchaguzi Unguja na Pemba. Katika mikutano hiyo, mambo
mbali mbali kuhusu Uchaguzi Mkuu yalijadiliwa. Pia Tume ilitangaza rasmi ratiba
ya Uchaguzi Mkuu.
• Tume ya Uchaguzi inaendelea na kazi ya mapitio ya
Idadi, mipaka na majina ya majimbo ya uchaguzi na inatarajia kutangaza majina
na mipaka mipya ya majimbo hayo baada ya kazi hiyo kukamilika.
• Tume ya Uchaguzi imekamilisha Kanuni za
Kura ya Maoni
na miongozo ya utoaji wa elimu ya uraia na elimu ya Wapiga Kura. Aidha, Tume
imetoa vibali kwa asasi za kiraia 61
kati ya asasi 75 zilizoomba kutoa elimu ya uraia kwa Zanzibar.
• Tume ya Uchaguzi imekamilisha uandaaji wa
Mpango wa Manunuzi ya Vifaa
(Procurement Plan) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu. Tume inatarajia kutangaza zabuni
ya ununuzi wa vifaa hivyo katika Mwezi
wa Mei, 2015.
• Tume ya Uchaguzi imefanya mapitio ya Sheria ya
Kura ya Maoni ya
mwaka 2010 ili kurahisisha utekelezaji wake.
• Tume kwa kushirikiana na “UN Women”, imeandaa rasimu ya Sera ya Ushirikishwaji wa
Makundi Maalum katika Uchaguzi (Gender Mainstreaming and Social Inclusion
Policy).
• Tume imefanya uchambuzi yakinifu wa mifumo
ya uandikishaji wa Wapiga Kura pamoja
na vifaa vya uandikishaji wa Wapiga Kura.
• Tume imeandaa Mpango wa Utekelezaji, Ratiba
ya Uchaguzi pamoja na Bajeti kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
• Tume imewapatia watendaji wake sita (6)
ziara ya mafunzo
ya siku tatu (3) nchini Kenya kwa ajili ya kujifunza masuala ya uendeshaji
wa uchaguzi.
• Tume ya Uchaguzi imewapatia mafunzo watendaji
wa Kitengo cha IT ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma kitaalamu. Aidha,
maandalizi yameanza ya kutengeneza upya Tovuti ya Tume pamoja na kuweka taarifa
mbali mbali zinazohusiana na uchaguzi.
46.0 Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Baraza lako Tukufu liliidhinisha jumla ya Shilingi 1,314,100,000 kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Hadi kufikia Machi, 2015
jumla ya Shilingi 1,229,926,569
zimepatikana na kutumika
kwa kazi za kawaida ambazo ni sawa na asilimia 94.
Utekelezaji Kifedha:
47.0 Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha
Miezi Tisa (Julai-Machi 2014/2015), Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ilipanga
kutumia jumla ya Shilingi 4,110,200,000 kwa
kazi za kawaida. Fedha zilizopatikana na kutumika ni shilingi 3,801,401,484 sawa na asilimia 92. Angalia Kiambatisho
Nam.1. Aidha, kwa upande
wa Miradi ya maendeleo Ofisi ilipanga kutumia jumla ya Shilingi 90,000,000 na hadi kufikia mwezi Machi jumla ya Shilingi 45,000,000 zimepatikana na kutumika sawa na asilimia 50 ya fedha zilizopangwa. Angalia Kiambatisho Nam. 2
48.0 Mheshimiwa
Spika, Baraza la
Wawakilishi katika kipindi hicho ilipanga kutumia Shilingi 14,564,000,000 kwa kazi za kawaida na fedha zilizopatikana ni Shilingi 13,954,901,100 sawa na asilimia 96. Angalia
Kiambatisho Nam. 1.
49.0 Mheshimiwa
Spika, Tume ya Uchaguzi
Zanzibar katika kipindi cha Miezi Tisa (Julai -Machi) 2014/2015 ilipanga
kutumia Shilingi 1,314,100,000 kwa kazi za kawaida na Fedha zilizopatikana ni Shilingi 1,229,926,569 sawa na asilimia 94. Angalia Kiambatisho Nam. 1.
Ukusanyaji wa
mapato:
50.0 Mheshimiwa
Spika, Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais inakusanya mapato kutoka
katika Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Idara ya Sherehe
na Maadhimisho ya Kitaifa na Idara ya Uendeshaji na Utumishi. Katika kipindi
cha Miezi Tisa (Julai- Machi 2014/2015), Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa
Mkuu wa Serikali ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi 450,000,000. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2014 Ofisi imekusanya jumla ya
Shilingi 295,903,000 sawa na asilimia 66 ya lengo. Aidha, kwa upande wa Idara ya Sherehe na
Maadhimisho ya Kitaifa ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi 2,250,000. Hadi kufikia mwezi wa Machi, 2015 imekusanya Shillingi 11,940,000 sawa na asilimia 530. Kwa upande wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi ilipangiwa
kukusanya Shilingi 3,750,000 ikiwa ni makusanyo
ya kodi ya ukumbi wa jengo la zamani la Baraza la Wawakilishi. Hadi kufikia
mwezi wa Machi, 2015, hakukuwa na fedha yoyote iliyokusanywa. Hali hii imetokana
na ukumbi huo kukosa kukodishwa kwa vile uko katika hali isiyoridhisha na
unahitaji matengenezo makubwa na kuwekwa vifaa vya kisasa. Angalia Kiambatisho Nam. 3
BAJETI KWA
MWAKA WA FEDHA 2015/2016
51.0 Mheshimiwa
Spika, Serikali inaendelea
kufanya mageuzi ya bajeti ikiwa ni sehemu ya mageuzi ya utawala na udhibiti wa
fedha za umma. Kwa mwaka huu wa fedha 2015/2016 Serikali imetoka katika mfumo
wa bajeti unaotumia vifungu (line item) na kwenda katika Mfumo wa Bajeti
unaotumia Programu.
52.0 Mheshimiwa
Spika, Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais na Taasisi zake ina Programu nane (8) na program ndogo 13 zinazohusisha malengo, na matokeo
yanayotarajiwa kupatikana katika program na program ndogo kama ifuatavyo:-
Programu ya Kwanza (C011):
Uratibu wa Shughuli za Makamu wa Pili wa Rais:
53.0 Mheshimiwa
Spika, lengo la Program
hii ni kuimarisha utendaji wa kazi kwa Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Pili wa
Rais. Matokeo yanayotarajiwa ni
kuimarika kwa Ofisi hii na kutoa huduma bora kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa
Rais. Huduma inayotolewa katika Ofisi ya Faragha ni kuratibu kazi mbali mbali
za Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais ikiwemo ziara za ndani na nje ya nchi,
mikutano na Mabalozi wa nchi mbali mbali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kitaifa na
Kimataifa na mikutano mbali mbali na wananchi kusikiliza kero na malalamiko
yao. Programu hii inatekeleza lengo la tatu katika klasta ya tatu ya MKUZA II
inayohakikisha ushirikishwaji wa wananchi katika Utawala wa Kidemokrasia.
Programu hii inatekelezwa na Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Pili wa Rais.
Programu ya
Pili (C012):
Uratibu wa
shughuli za Serikali:
54.0 Mheshimiwa
Spika, Program hii lengo
lake kubwa ni kuweka mfumo imara na endelevu kwa Uratibu wa Shughuli za
Serikali. Programu hii inatekeleza lengo la tatu katika klasta ya tatu ya MKUZA
II la kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi katika utawala wa kidemokrasia.
Aidha, Programu hii ina programu ndogo tatu zifuatazo:-
i. Programu
Ndogo (C0121): Uratibu wa Shughuli za Kukabiliana na Maafa.
55.0 Mheshimiwa
Spika, Programu hii ndogo
lengo lake kuu ni kujenga uhimili kwa jamii katika kukabiliana na maafa.
Matokeo yanayotarajiwa ni kutoa huduma bora kabla, wakati na baada ya maafa.
Huduma inayotolewa ni Uratibu wa Shughuli mbali mbali za kukabiliana na maafa
ikiwemo kutoa mafunzo kwa jamii, kuwahudumia waathirika wa majanga na maafa na
kuandaa na kutoa miongozo mbali mbali inayosimamia utekelezaji wa kazi za
maafa. Programu hii ndogo inatekelezwa na Idara ya Kukabiliana na Maafa.
ii. Programu
Ndogo (C0122): Uratibu wa Shughuli za Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja
na Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa.
56.0 Mheshimiwa
Spika, Programu hii ndogo
lengo lake ni kuwa na sherehe zenye hadhi na kudumisha historia na kumbukumbu
za Viongozi Wakuu wa Kitaifa. Matokeo yanayotarajiwa ni ubora na ufanisi wa
sherehe na maadhimisho ya kitaifa na kuwa na kumbukumbu zenye kuelezea historia
za Viongozi Wakuu wa Kitaifa. Huduma inayotolewa ni Uratibu wa shughuli za
Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja na Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa. Programu hii ndogo inatekelezwa na Idara ya
Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa.
57.0 Mheshimiwa
Spika, lengo kuu la Programu
hii ndogo ni kuimarika kwa utekelezaji wa shuguli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
mambo ya Muungano na Uratibu wa Shughuli za Serikali, Dar es Salaam kupitia
sekta mbali mbali. Matokeo yanayotarajiwa ni kuwa na utekelezaji wa ufanisi kwa
malengo ya Serikali. Huduma inayotolewa ni Uratibu wa Shughuli za Serikali
(SMZ) ikiwemo kukusanya taarifa za utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Programu hii ndogo inatekelezwa na Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali
Zanzibar na Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Dar es Salaam.
Programu ya Tatu (C013): Usimamizi wa Shughuli za
Upigaji Chapa.
58.0 Mheshimiwa
Spika, lengo kuu la
Progrmu hii ni kuimarisha huduma za upigaji chapa. Matokeo yanayotarajiwa ni
kutoa machapisho bora na kwa wakati. Kiwanda cha Upigaji Chapa kinatoa huduma
za kuchapisha nyaraka mbalimbali za Serikali zikiwemo Hotuba za Bajeti za
Wizara mbali mbali, vyeti vya kuzaliwa, Gazeti Rasmi la Serikali, Miswada ya
Sheria na Sheria na Machapisho mengine. Programu hii inatekeleza lengo la Tatu
katika klasta ya Tatu ya MKUZA II la kuhakikisha uimarishaji wa Demokrasia na
Utawala bora. Programu hii inatekelezwa na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali.
Programu ya
Nne (C014): Mipango na Utawala.
59.0 Mheshimiwa Spika, lengo la Programu hii ni kuimarisha mazingira bora ya
wafanyakazi na usimamizi wa shughuli za Ofisi. Matokeo yake ni kuimarika kwa
utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wafanyakazi na wadau mbali mbali wa
Ofisi hii. Programu hii itatekeleza lengo la tatu katika klasta ya tatu ya MKUZA
II la kuimarisha utawala wa sheria wenye kuheshimu haki za binaadamu na
upatikanaji wa haki za sheria. Programu hii ina Programu ndogo tatu (3)
zifuatazo:-
i. Programu
ndogo (C0141): Uongozi na Utawala.
60.0 Mheshimiwa
Spika, Programu hii ndogo
ina lengo la kuimarisha na kusimamia utendaji kazi katika Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais. Matokeo yanayotarajiwa ni matumizi bora ya rasilimali,
wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu na ufanisi katika utendaji kazi. Huduma zinazotolewa ni kutoa huduma za Utumishi
na Uendeshaji, ikiwemo stahiki mbali mbali na kuwapatia mafunzo na vitendea
kazi wafanyakazi. Programu hii ndogo inatekelezwa na Idara ya Uendeshaji na
Utumishi.
ii. Programu
ndogo (C0142): Mipango, Sera na Utafiti.
61.0 Mheshimiwa
Spika, Programu hii ndogo
ina lengo la kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mipango na Bajeti na
kufuatilia utekelezaji wa Program/Miradi ya Maendeleo ya Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais. Matokeo yanayotarajiwa ni kuwa na mipango endelevu na yenye
kuleta maendeleo. Huduma inayotolewa ni kuratibu uandaaji na kusimamia
utekelezaji wa mipango, sera na bajeti. Programu hii ndogo inatekelezwa na
Idara ya Mipango Sera na Utafiti.
iii. Programu
ndogo (C0143): Ofisi Kuu Pemba.
62.0 Mheshimiwa Spika, lengo kuu la Program hii ndogo ni kuimarisha mazingira
bora ya kufanyia kazi na usimamizi wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais Pemba. Matokeo yanayotarajiwa ni utendaji na utekelezaji wa kazi za Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba kwa ufanisi. Huduma inayotolewa ni kuratibu
kazi zote za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Pemba.
63.0 Mheshimiwa
Spika, vile vile Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais inaratibu shughuli za Baraza la Wawakilishi na Tume ya
Uchaguzi ambazo nazo zina Programu Kuu na Programu Ndogo kama ifuatavyo:-
Baraza la
Wawakilishi:
64.0 Mheshimiwa
Spika, Baraza la
Wawakilishi lina Program mbili (2)
Programu ya kwanza (C021): Kutunga
Sheria, kupitisha Bajeti na kusimamia Taasisi za Serikali:
65.0 Mheshimiwa
Spika, lengo la Programu
hii ni kuhakikisha haki na utawala wa sheria unatelekelezwa Zanzibar. Matokeo
yanayotarajiwa ni kukua kwa demokrasia na uwakilishi wa wananchi. Programu hii
itatekeleza lengo la tatu katika klasta ya tatu ya MKUZA II la kuimarisha
utawala wa sheria wenye kuheshimu haki za binaadamu na upatikanaji wa haki za
sheria. Huduma zinazotolewa ni kujadili, kurekebisha na kupitisha miswada ya
Sheria, kusimamia utendaji wa taasisi za Serikali na kupitisha bajeti ya
Serikali.
Programu ya Pili (C022): Uongozi na Utawala wa
Baraza la Wawakilishi:
66.0 Mheshimiwa
Spika, lengo la Programu
hii ni kuweka mazingira mazuri ya kazi, kuwajengea uwezo Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi na wafanyakazi wa Ofisi ya Baraza. Matokeo yanayotarajiwa ni
kuongezeka kwa ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Ofisi kwa ufanisi.
Programu hii itatekeleza lengo la tatu katika klasta ya tatu ya MKUZA II la
kuimarisha utawala wa sheria wenye kuheshimu haki za binaadamu na upatikanaji
wa haki za sheria. Huduma zinazotolewa ni kuwapatia Wajumbe na wafanyakazi wa
Baraza huduma na stahiki zao, kuimarisha uwezo wa Wajumbe na watendaji na
kuimarisha mazingira ya kazi ya Ofisi ya Baraza.
Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar:
67.0 Mheshimiwa
Spika, Tume ya Uchaguzi
ina Program mbili (2) na Programu ndogo tatu (3)
Programu ya Kwanza (C031): Uendeshaji wa Shughuli za
Uchaguzi.
68.0 Mheshimiwa
Spika, lengo la Programu
hii ni kukuza demokrasia na umoja wa kitaifa. Matokeo yanayotarajiwa ni kuwa na
Uchaguzi huru na wa haki na wenye kufuata misingi ya kisheria. Programu hii
itatekeleza lengo la tatu katika klasta ya tatu ya MKUZA II la kuimarisha
utawala wa sheria wenye kuheshimu haki za binaadamu na upatikanaji wa haki za
sheria. Huduma zinazotolewa ni kufanya Uchaguzi Mkuu, Chaguzi ndogo na Kura ya
maoni, Kufanya Uchambuzi wa Idadi, Majina na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi,
Kuratibu na kutoa Elimu ya Wapiga Kura na Uandikishaji wa Wapiga Kura na
Uendelezaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Programu ya Pili (C032): Usimamizi
wa Kazi za Utawala na Uendeshaji wa Shughuli za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
69.0 Mheshimiwa Spika, lengo la Programu hii ni kuimarisha Usimamizi wa mwenendo
wa Shughuli za Uchaguzi. Matokeo yanayotarajiwa ni uendeshaji bora wa kazi za
Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Programu hii itatekeleza lengo la tatu
katika klasta ya tatu ya MKUZA II la kuimarisha utawala wa sheria wenye
kuheshimu haki za binaadamu na upatikanaji wa haki za sheria. Programu hii ina
Programu ndogo mbili (2) zifuatazo;
i. Programu
ndogo (C0321): Usimamizi wa kazi za
Utawala na Uendeshaji wa Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
70.0 Mheshimiwa
Spika, lengo la Programu
hii ndogo ni kuimarisha Usimamizi wa mwenendo wa Shughuli za Uchaguzi. Matokeo
yanayotarajiwa ni uendeshaji bora wa Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Huduma zinazotolewa na program hii ndogo ni kuimarisha mazingira bora ya
kufanyia kazi, kuimarisha maslahi ya wafanya kazi na kuwajengea uwezo
wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
ii. Programu
ndogo (C0322): Usimamizi
wa kazi za Utawala na Uendeshaji wa Ofisi Ndogo ya Tume ya Uchaguzi Pemba.
71.0 Mheshimiwa
Spika, lengo la Programu
hii ndogo ni kuimarisha Usimamizi wa mwenendo wa Shughuli za Uchaguzi. Matokeo
yanayotarajiwa ni uendeshaji bora wa Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Huduma zinazotolewa na program hii ndogo ni kuimarisha mazingira bora ya
kufanyia kazi ya Tume ya Uchaguzi Pemba. Kwa muhtasari wa Programu na Programu
ndogo za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Taasisi zake Angalia Kiambatisho Nam. 4
MGAO WA FEDHA
KWA PROGRAMU:
72.0 Mheshimiwa
Spika, mgao wa fedha kwa
Programu za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Taasisi zake ni kama ifuatavyo:-
Programu: Uratibu wa Shughuli za Makamu wa Pili wa Rais. Programu hii
inatekelezwa na Ofisi ya Faragha ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais. Jumla ya
Shilingi 625,569,000 zimepangwa kwa ajili ya kufanikisha programu.
Programu: Uratibu
wa Shughuli za Serikali: Programu hii inajumuisha Idara ya Kukabiliana na
Maafa, Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa, Idara ya Uratibu wa Shughuli
za Serikali na Idara ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es Salaam. Jumla ya
Shilingi 2,239,727,000
zimepangwa kwa ajili ya
kufanikisha program hii.
Programu: Usimamizi wa Shughuli za Upigaji Chapa: Programu hii
inatekelezwa na Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali. Jumla
ya Shilingi 714,050,000 zimepangwa kwa ajili ya kufanikisha program hii.
Programu: Mipango
na Utawala. Programu hii inajumuisha Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Idara ya
Mipango, Sera na Utafiti na Ofisi Kuu Pemba. Jumla ya Shilingi 1,587,354,000 zimepangwa kwa ajili ya kufanikisha program hii.
73.0 Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, mgao wa fedha kwa
Programu ni kama ifuatavyo:-
Programu: Kutunga
Sheria, kupitisha bajeti na kusimamia Taasisi za Serikali. Makisio ya fedha kwa
program hii ni Shilingi 6,539,295,000
zimepangwa kwa ajili ya kufanikisha program hii.
Programu: Uongozi na Utawala
wa Baraza la Wawakilishi. Programu hii inajumuisha kazi za utawala kwa Baraza
la Wawakilishi Unguja na Pemba. Jumla ya Shilingi 10,223,305,000 zimepangwa kwa ajili ya kutekeleza program hii. Angalia Kiambatisho Nam. 5
74.0 Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar, mgao wa fedha kwa Programu ni kama ifuatavyo:-
Programu: Uendeshaji wa Shughuli za
Uchaguzi. Makisio ya fedha kwa program hii yanaainishwa katika Mfuko Mkuu wa
Serikali.
Programu:
Usimamizi wa Kazi za Utawala na Uendeshaji. Programu hii inajumuisha kazi za
utawala kwa Tume ya Uchaguzi Unguja na Pemba. Jumla ya Shilingi 1,404,000,000 zimepangwa kwa ajili ya kutekeleza programu hii.
75.0 Mheshimiwa
Spika, jumla ya gharama
kwa Programu zote za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Baraza la Wawakilishi na
Tume za Uchaguzi Zanzibar ni Shilingi 23,333,300,000.
UKUSANYAJI
MAPATO:
76.0 Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa
mapato kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imepanga
kukusanya mapato ya jumla ya Sh. 612,360,000 kwa mchanganuo ufuatao:-
Idara ya Upigaji Chapa na
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Sh. 600,000,000
Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya
Kitaifa Sh. 12,360,000
Jumla Sh. 612,360,00
HITIMISHO:
77.0 Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa
Mohamed Aboud Mohamed, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa
kunisaidia kutekeleza majukumu yangu kwa ufanisi mkubwa. Aidha, nawashukuru kwa
dhati watendaji na wafanyakazi wote wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na
Taasisi zilizo chini ya Ofisi hii wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. Khalid Salum
Mohamed na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Ahmad Kassim Haji kwa juhudi zao katika
kutekeleza majukumu yao.
78.0 Mheshimiwa
Spika, natoa shukrani
zangu za dhati kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, na shukrani maalumu kwa
Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu
wa Kitaifa kwa mashirikiano, ushauri na maelekezo waliyotupa katika kipindi chote cha miaka mitano
iliyopita ambayo yalitusaidia sana katika kufanikisha majukumu yetu.
Aidha, napenda kuwashukuru sana Washirika wetu wa Maendeleo
wote (Development Patners) na nchi marafiki ambazo zinaendelea kuchangia katika
kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Ofisi yangu na ya nchi kwa jumla katika
mwaka wa fedha 2014/2015. Miongoni mwao ni: Benki ya Dunia, Clinton Foundation,
China, FAO, Finland, Norway, India, Japan, Marekani, Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Kifua Kikuu Malaria na UKIMWI (Global Fund), Oman, UNAIDS, USAID,
UNDP, UNICEF, UNFPA, WHO, WFP na WIPO.
Vile vile, naishukuru sana Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Tanzania na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ushirikiano wao mkubwa na Ofisi
yangu. Pia, nazishukuru Taasisi zisizo za Kiserikali, Jumuiya ya Wafanya biashara,
Wenye viwanda na Wakulima kwa kuendelea kuisaidia Serikali katika kutoa huduma
za jamii na kuleta maendeleo katika nchi yetu. Pia nawashukuru sana wananchi
wote ambao wamefuatilia na kusikiliza hotuba yangu hii.
79.0 Mheshimiwa
Spika, baada ya maelezo
hayo, sasa naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya 23,333,300,000 kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Taasisi zake (Tume
ya Uchaguzi na Bazara la Wawakilishi).
Kwa ajili ya kutekeleza Programu mbali mbali nilizozielezea hapo juu.
Mchanganuo halisi wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:
i.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shs: 5,166,700,000
ii.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Shs:
1,404,000,000
iii.
Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Shs:
16,762,600,000
Jumla:
Shs: 23,333,300,000
80.0 Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
No comments:
Post a Comment