Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Zenj.

Na Rahma  Khamis  Maelezo - Zanzibar  20/5/2015
Serikali inakusudia kuimairisha zaidi huduma za usafi wa Mji kwa kuvishirikisha vikundi vya jamii  na mazingiara(CBOsna NGOs ) na taasisi za Serikali, Binafsi kwa  kuwahamasisha Wananchi  kwa kushiriki na kutunza gharama za usimamiaji huduma za usafi wa Mji kwa mujibu wa Sheria na kanuni za Manispaa.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheri huko Chukwani  Baraza la Wakilishi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar alipokua akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub alipotaka kujua Serekali imetumia kiasi gani cha gharama za kuweka usafi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar

Amesema Serikali inaendelea na juhudi mbalimbali hivi sasa katika kuhakikisha suala la usafi wa Mji huo na unaimarishwa licha ya kupatikana kwa vifaa muhimu kupitia mradi unaoendelea(ZUSP) ikwemo magari na makontena.

Aidha amesema Baraza la Manispaa limejifunza mengi katika kipindi cha maandalizi ya Rais wa Ujerumani jambo ambalo limetoa mashirikiano na uwajibikaji katika kuhakikisha usafi wa Mji unaimarika.

“Tumejifunza kuwa na mashirikiano ya pamoja kwa kila Taasisi kuwajibika kwa upande wake tunaweza kuhakikisha Mji wetu kuwa msafi kwa gharama ndogo zaidi”alisema Waziri Haji

Hata hivyo Serekali imeweka makalbi katka Bandari ya Malindi kuelekea Forodhani kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari kwa kuheshimu taratibu za urithi wa Mji Mkongwe ili uweze kuvutia zaidi.

Sambamba na hayo katika kuimarisha usafi huo Baraza la Manispaa lilipokea TZS 2,500,000/= kutoka Serekali kuu kupitia kamati ya kitaifa ya sherehe na mapambo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili Rais kwa nia ya kusaidia Baraza katika kuimarisha usafi wa Mji ili uweze na kuvutia.
                                        
Na Mwanaisha Mohd -Maelezo.
Mahakama ya Chake Chake Pemba imewatia hatiani wafanyakazi  wawili wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) baada ya kufanya ubadhilifu  wa  Tshs 19.2milioni mali ya Shirika la Umeme na kutakiwa kuzilipa fedha hizo  .

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee huko Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa jimbo la Wawi Nassor Juma alipotaka kujua sababu zilizopekekea  wafanyakazi kufukuzwa kazini.


Amesema uongozi wa (ZRB)umewafukuza wafanyakazi hao baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la jinai (Wizi)  kwa mujibu wa kifungu cha 84cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2011 na kanuni za Utumishi za mwaka 2002 kifungu 69 (3)  na kutakiwa kulipa fedha hizo  pamoja na faini ndani yake kwa kipindi cha miezi miwili.

Akizitaja sababu za kufunguzwa  Waziri  Omar Yussuf amesema kwamba   ni kosa la kula njama kinyume na Sheria ya Namba 6 ya mwaka 2004ya Sheria ya Zanzibar

Hata hivyo Waziri huyo  amesema sababu nyengine za kufukuzwa ni kutengeneza hati ya uongo kinyume na kifungu 340 (d) (1) na kifungu cha 342(2) ya Sheria ya namba 6ya mwaka 2014 kwa  Sheria ya Zanzibar.

Akijibu swali la nyongeza Waziri huyo ameeleza kuwa  fedha hizo zimeshaanza kulipwa  na kuna muelekeo wa kumaliza kwani  muda waliopewa na Mahakama hiyo ni mfupi (miezi miwili).

Sambamba na hayo Mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wenye tabia kama hizo.

Na Miza Othman- Maelezo.
Serikali ya awamu ya saba imechukuwa hatuwa mbambali za kuimarisha huduma za Elimu, Afya,Majisafi na salama pamoja na Makaazi ili kuleta ustawi mzuri kwa jamii.

 Hayo yameeelezwza leo na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwasilisha hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi  ya Makamu wapili wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 huko Chukwani  katika Ukumbi wa  Baraza la Wawakilishi  nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema  Serikali imeendelea kuchukuwa hatuwa madhubuti ya kuimarisha na kuendeleza elimu ikiwemo ujenzi wa Skuli  na Madarasa mapya kwa Skuli za Maandalizi Msingi na Sekondari, pamoja na Ununuzi wa Vitabu vya ziada katika Skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.

Balozi Seif amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo Walimu kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa lengo la kuimarisha ubora wa Elimu inayotolewa Maskulini humo.

Aidha amesema pia Serikali itaendelea kuimarisha huduma za kinga na Tiba katika Hospitali na Vituo vya Afya sambamab na kutowa Elimu ya Afya kwa Wananchi kwa lengo la kujikinga na maradhi ya kuambukiza na yasioambukiza.

Hata hivyo amesema Serikali imezifanyia matengenezo makubwa Hospitali na Vituo vya Afya na kujenga Majengo mengine mapya Unguja na Pemba ikiwemo Wodi ya wagonjwa mahatuti (ICU) na kitengo cha huduma za upasuwaji Vichwa na Uti waMgongo (Neuro Surgical Unit) katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Vile vile Serikali imechukuwa Madaktari na Wahudumu wengine wa Afya kwa kuwasomesha na kuwapatia uzowefu kutokana na  Nchi kwani hivi sasa inamadaktari wazalendo.

“Hivi sasa Nchi yetu inamadakatari  wazalendo wapatao 44 na Madaktari Bingwa wazalendo 13”, amesema Balozi Seif .

Kutokana na hali hiyo Serikali imesema  kwamba imeshawapatia Madaktari wa Maradhi mbali mbali kwa lengo la kuwahudumia Wananchi kwa kushirikiana na Nchi marafiki.

     IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.