Habari za Punde

Kutohudhuria vikao vya BLW: Watendaji SMZ hubanwa na majukumu ya kazi

Na Kijakazi Abdalla / Mariam Kidiko -Maelezo Zanzibar.
 
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohamed Aboud Mohamed amesema kuwa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hawafanyi kwa makusudi kutohudhuria katika vikao vya baraza la Wawakilishi za  Wizara zao ila baadhi ya wakati wanadharura kutokana na kubanwa na majukumu ya kazi.
 
Hayo yameelezwa huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar katika kikao cha baraza la Wawakilishi wakati akijibu suali la Mwakilshi wa Jaku Hashim Ayuob wa Jimbo la Muyuni..
 
Alisema kuwa baadhi ya Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarwanaoshindwa kuhudhuria wakati wa kipindi cha maswali na majibu barazani huwa wanabanwa na majukumu ya kazi na wakati mwengine wanakuwa safarini nje ya Zanzibar.
 
Aidha alisema kwa ujumla watendaji wanaajibika ipasavyo katika kuwasaidia viongozi (Waheshimiwa Mawaziri) kwa kuwatayarishia majawabu sahihi ya maswali yanayohusu Wizara zao
 
Sambamba na hayo Mhe Waziri alisema Serikali itachukuwa juhudi ya kuwakumbusha watendaji  wote kutimiza wajibu wao wa kuhudhuria vikao vya baraza la Wawakilishi katika kipindi cha maswali na majibu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.