Habari za Punde

Kutoka Baraza la wawakilishi: Wagonjwa wa ukoma hawatengwi na familia zao

Na Kijakazi Abdalla / Mariam Kidiko -Maelezo
 
Wizara ya Afya  imesema  Wagojwa wa Ukoma hawatengwi na Familia zao kasababu Dawa wanazotumia zinauwezo mkubwa za kutibu na kuuwa vimelea kwa wingi na kwa muda na hatimae kupungua maambukizi.
 
Akijibu swali la muwakilishi  Mohammed Haji Khalid (Jimbo la Mtambile) katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani  nje kidogo wa Mji wa Zanzibar Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe Mahmoud Thabit Kombo .
 
Alisema kuwa hapo zamani Watu waligunduliwa na maradhi ya Ukoma walikuwa wakipelekwa katika Kambi maalum kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Kambi hizo kwa Unguja walipelekwa Welezo na Pemba Makondeni.
 
Aidha alisema kwa zamani walipokuwa wakitegwa walikuwa wanatumia Dawa kwa muda usiopunguwa miaka mitano au zaidi ya hali ya uponeshaji ulikuwa mdogo.
 
Alisema kuwa baada ya hapo palitumika Dawa mseto aina ya (MDT) zilitumika ambazo zinauwezo wa kukatisha maambukizi kwa muda mfupi ;
 
Sambamba na hayo Naibu Waziri huyo ameishauri Jamii kutowatenga au kuwanyanyapaa Wagojwa wa maradhi ya Ukoma au wale wenye ulemavu uliotokana na Ugojwa huo.
 
Hata hivyo amewataka Baadhi ya Watu  kuwaelimisha  wale wenye dalili kujitokeza katika Vituo vya Afya ili watibiwe mapema na kuepuka  Ulemavu utokanao na Ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.