Habari za Punde

Maonesho ya Mafanikio ya Mradi wa SMOLE 2. Zanzibar

Afisa Idara ya Misitu Zanzibar Bi. Miza Suleiman akitowa maelezo kuhusiana na mradi wa SMOLE kuhusiana na mazingira ya misitu Zanzibar.
Afisa wa Upimaji Ardhi Zanzibar Ndg Alamin Omar akitowa maelezo ya jinsi ya upimaji wa Ardhi kupitia Mradi wa SMOLE 2, wakati wa maonesho ya kutowa mafanikio ya mradi huo katika sekta hiyo. 
Afisa wa Mipango Mji Ndg,Said S.Ufuzo akitowa maelezo wakati wa maonesho hayo ya kutowa tathimini ya mafanikio ya Mradi wa SMOLE 2 katika utafiti wa Mipango Mji, maonesho hayo yamefanyika katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar. kulia Balozi wa Finland Tanzania Balozi Sinikka Antila, Mkurugenzi Mipango Miji na Vijini Dk Mohammed Juma na Wiziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Fatma Ferej.   
Mkurugenzi Mipango Mji na Vijiji Dk Mohammed Juma akitowa maelezo ya mafanikio ya Mradi wa SMOLE 2 kwa Balozi wa Finland Tanzania Balozi Sinikka Antla wakati wa maonesho ya ufungaji wa mradi wa smole Zanzibar yaliofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.