Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe Fatma Ferej akiwasilisha hutuba ya Bajeti ya Wizara yake katika Kikao cha Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar wakifuatilia Hutuba ya Bajeti ya Ofisi yao wakati ikiwasilishwa na Waziri Mhe Fatma Ferej. wakati wa Kikao cha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015-2016
Wakurugenzi wa Idara za Ofisi za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wakifuatilia Bajeti hiyo kupitia Vitabu vya Bajeti wakati ikiwasilishwa katika Kikao cha Bajeti.

                        Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakibadilishana mawazo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mohammed Mussa wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana. 
                          Wajumbe wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano wakibadilishana mawazo baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bajeti cha asubuhi kwa ajili ya mapumziko ya mchana.
Maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wakitoka katika ukumbi wa Mkutano wa Jengo la Baraza la Wawakilishi baada ya kuwasilishwa Bajeti ya Ofis yao na kujadiliwa na kupitishwa. na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.