Habari za Punde

Maonesho ya Wafanyakazi ya Mei Mosi Viwanja vya Maisara Zenj.

WANANCHI wakipata maelezo kutoka kwa Mwabnafunzi wa Mwaka wa Pili Thuwaiba Thani wa Zanzibar School of Heath, Chuo cha Afya, wakati wa maenesho ya Mei Mosi yanayofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar , akitowa maelezo jinsi ya mtoto anavyokuwa tumboni mwa mama.
WANANCHI wakiangalia miche ya aina mbali mbali ya miti ya matunda walipofika katika banda la maonesho la JKU, kujionea kazi za Vijana wa Jeshi la Kujenga Uchumi, katika viwanja vya maisara jana.
MWANAFUNZI wa Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya  Afya Zanzibar,  akitowa maelezo kwa wananchi waliofika katika banda hilo, jinsi ya kutambua kwa bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi yake kwa mlaje na madhara yanayopatikana kwa matumizi ya Vyakula hivyo.
AFISA wa Idara ya  Uhamiaji Zanzibar,Sharif Bakari, akitowa maelezo kwa Wananchi waliotembelea banda la Uhamiaji katika viwanja vya maonesho ya mei mosi, akitowa maelezo ya jinsi ya huduma zinazotolewa nas Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
Mkurugenzi wa ZANEMA Salah Salim Salah, akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa ZSTC Issa Hamadi, wakati alipotembelea banda hilo baada ya kuyafungua Maonesho ya Wafanyakazi ya Mei Mosi katika viwanja vya KMKM Maisara Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.