Habari za Punde

Ujumbe wa Skuli ya Sekondari ya Kusini wawasili Sweden kwa ziara ya siku 10

Ujumbe wa Skuli ya Sekondari ya Kusini umewasili nchini Sweden kwa ziara ya siku 10 ya masomo kufuatia mualiko wa rafiki zao Skuli ya Sundsvall Gymnasium iliyopo mji wa Sundsvall. 

Ujumbe huo umeongozwa na mwalimu Suleiman Pandu Hassan mwenye fulana jeupe na kofia, akisaidiwa na mwalimu Fatma Ali Haji na mwalimu Aboud Simai. 

Hii ni mara ya tatu kwa walimu na wanafunzi wa Skuli ya Kusini kupata fursa ya kwenda Sweden kujifunza mambo mbali mbali ya kitaaluma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.