Habari za Punde

Innaa Lillaahi wainnaa ilayhi Raaji'uun: Sheikh Mkuu , Mufti Shaaban Simba amefariki


1 comment:

  1. Allah amsamehe makosa yake na ampumzishe mahala pema peponi amin!

    Wengi tutakumbuka kwamba moft Simba aliongoza BAKWATA ktk. zama zenye changamoto nyingi kwa kutumia mbinu za kizamani.

    Kwa mfano: alipokua akilalamikiwa na Waislamu wa Bara kwamba wanatengwa ktk fursa za ajira yeye majibu yake yalikua "Na nyinyi someni" bila kujua maskini kwamba Tza ya leo karibia jamii zote zimesoma isipokua tu zinatofautiana kwa idadadi ya wasomi wenyewe!

    Wakati taasisi za wenzetu zinakwenda nje kuingia mikataba na taasisi za huko kuja kujenga vyuo vikuu, mahospitali, mabenki nk. ambavyo huvitumia kibiashara na kunufaisha waumini wao yeye alikua anakwenda kuomba kujengewa miskiti tu!

    Wakati taasisi za wenzetu zinachambua siasa ya nchi na kutoa waraka wa aina ya rais wanaemtaka yeye alikua akikemea wafuasi wake kuchanganya Dini na siasa!

    Wakati taasisi za wenzetu zinaimarisha mshikamano baina yao bila kujali madhehebu, taasisii yake iliimarisha mpasuko baina ya madhehebu za kiislamu, vile wanaotangulia kufunga na wanaochelewa, kanzu fupi na ndefu, wenye ndevu na wasio na ndevu, siasa kali na siasa poa na hatimae wale wote wasiokua BAKWATA kujikuta matatani!

    Hata hivyo,Mufti ameondoka ktk kipindi ambacho tulikua tunamuhuitaji mno ili atusaidie ktk juhudi za upatikanaji wa mahakama ya kadhi juhudi ambazo ndie aliezianzisha!

    Tumuombee kheri mzee wetu!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.