Habari za Punde

Maadhimisho ya miaka 23 ya ZLSC tawi la Pemba

 WANAFUNZI wa kituo cha kulea watoto Mayatima cha African Muslims Agency Mabaoni Chake Chake Pemba, wakishusha baadhi ya misada iliyotolewa na kituo cha Huduma za Sheria Tawi la Pemba, kwa watoto hao katika maadhimisho ya miaka 23 tokea kuanzishwa kwa ZLSC Zanzibar.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)
 AFISA Mipango wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba (ZLSC) Halfan Amour, akibeba kipolo cha mchele ikiwa ni miongoni mwa misaada waliotoa kwa watoto mayatima wanaolelewa katika kituo cha Africa Muslims Agency huko Mabaoni Chake Chake Pemba, baada ya ZLSC kutimiza miaka 23.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)
 MRATIB wa kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ofisi ya Pemba, Fatma Khamis Hemed, akimkabidhi msimamizi wa Africa Muslims Agency mabaaoni Chake Chake Pemba, ikiwa ni maadhimisho ya ZLSC kutimiza miaka 23 tokea kuanzishwa kwake.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)
 WAFANYAKAZI wa kituo cha Huduma za sheria Zanzibar (zlsc) Ofisi ya Pemba, wakiwa elekea wodi ya watoto kutoa zawadi katika hospitali ya Chake Chake kuwapatia zawadi, ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 23 kuanzishwa kwa kituo hicho.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)

 DAKTARI Dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Dk Yussuf Hamad Iddi, akiwawakaribisha watendaji wa kituo cha Huduma za sheria Zanzibar (ZLSC) Ofisi ya Pemba, katika wodi ya watoto kwa lengo la kuwapatia msada wao, ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 23 kwa kituo hicho.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)
 MRATIB wa Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar ofisi ya Pemba, Fatma Khamis Hemed akimpatia zawadi ya biskuti, mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto ndani ya Hospitali ya Chake Chake ikiwa ni Maadhimisho ya kutimiza miaka 23 kuanzishwa kwa kituo hicho.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)
 MRATIB wa KItuo Cha Huduma za sheria Zanzibar Ofisi ya Pemba, Fatma Khamis Hemed akimkabidhi Daktari dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Dk Yussuf Hamad Iddi, vifaa mbali mbali ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 23 kwa kituo hicho.(Picha na AbdI Suleiman, PEMBA.)
WAFANYAKAZI wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ofisi ya Pemba, wakijumuika katika chakula cha mchana na mjumbe wao wa bodi wa ZLSC Daudi Othamna Kondo wa pili kutoka kushoto, ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 23 kwa kituo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.