Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akimueleza jambo Mkurugenzi wa Kituo cha Kukuza Utalii kati ya India na Zanzibar Jilesh Babla (hayupo pichani) walipokuwa na mazungumzo Ofisini kwake Kikwajuni.(Picha Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
Waandishi wa Habari wakifuatilia habari hizo kwa makini katika Ofisi ya Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar.( Picha Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
Mkurugenzi wa wa Kituo cha Utalii kati ya India na Zanzibar Jilesh Babla akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Joseph Kilangi wakati wa mazungumzo hayo.(Picha Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
Picha ya pamoja ya Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk (katikati) pamoja na Mgeni wake Jilesh Babla (kushoto) na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara hiyo Joseph Kilang.(Picha Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
Mwashungi Tahir na Maryam Kidiko, Maelezo
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Saidi Ali Mbarouk amewataka wananchi wa Zanzibar na hasa waongozaji wa watalii kujifunza lugha ya kihindi ili waweze kuwahudumia watalii kutoka nchi hiyo ambao wanatarajiwa kutembelea Zanzibar kwa wingi hivi karibuni.
Hayo ameyasema leo huko ofisini kwake Kikwajuni wakati alipokuwa na mazungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kukuza Utalii kati ya India na Zanzibar Jilesh Babla.
Amesema kufunguliwa kwa kituo cha kukuza utalii katika Mji wa Mumbai nchini India, Zanzibar itapokea wageni wengi ambao watahitaji huduma muhimu za mawasiliano wakiwa nchini.
Amesema kuanzia msimu ujao wa utalii unaoanza mwezi wa Juni wanakadiriwa kupata kiasi cha Watalii 500 kutoka India na watahitaji huduma mbali mbali.
“Miezi michache ijayo tunatarajia kupokea watalii makundi kwa makundi wakiwemo kutoka India na hii ni ishara njema ya kuwepo mashirikiano mazuri kati ya Zanzibar na India,” alisema Saidi Ali Mbarouk.
Nae Mkurugenzi wa Utangazaji wa Utalii Mumbai Jilesh Babla amesifu mashirikiano mazuri yaliyopo baina ya Ofisi yao iliyopo mjini Mumbai na Wizara ya Habari ambayo yataanza kuleta mafanikio muda mfupi ujao.
Ameyataja mashirika ya ndege ya Kenya, Oman, Ethiopia na Italy ambayo mashirika watashirikiana nayo ili kuweza kuleta watalii jambo ambalo litaweza kurahisisha shughuli za kitalii hapa nchini na kuleta faraja kubwa.
Mr Babla aliziomba hoteli za Zanzibar kujitokeza kwa wingi ili waweze kujitangaza na kuweza kujulikana ili watalii watapokuja waweze kuyafahamu yale mahoteli
Sambamba na hayo mkurugenzi huyo aliomba kuwepo mashirikiano makubwa kati ya wafanya biashara wa India na Zanzibar ili kuweza kupata maendeleo visiwani humu.
perfect
ReplyDelete