Habari za Punde

Makamu wa Rais DKT.Bilal Aongoza Wananchi wa Ukonga kwenye Mazishi ya Mbunge wa Jimbo Hilo Marehemu EUGEN MWAIPOSA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugen Maiposa kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Juni 06, 2015 nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho kwenye Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugen Mwaiposa aliyefariki Ghafla nyumbani kwake Dodoma juzi, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo Juni 06, 2015 nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekua Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugen Mwaiposa wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugen Mwaiposa baada ya mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam leo Juni 06, 2015. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.