Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako
Manongi na Christopher Grima Malta wakitia sahihi hati za kuanzisha
uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya
Mabalozi. Wanaoangalia utiaji sahihi
ni Tully Mwaipopo Afisa
Mwandamizi wa Uwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania na Bw. Alan Cordina, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Malta
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Mwakilishi wa Kudumu wa Malta katika Umoja wa
Mataifa, Balozi Christopher Grima wakipongezana mara
baada ya kutia sahihi hati
walizoshika za kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya
Mabalozi. Hati hizo baadaye ya zitawasilishwa
rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya
Malta zimekubaliana kuanzisha uhusiano
wa kidiplomasia baina yao.
Wawakilishi
wa Kudumu wa mataifa hayo mawili katika
Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi wa Tanzania na Christopher Grima wa
Malta ndio waliotia sahihi hati za kuridhia kuanzishwa kwa uhusiano huo na ambao utakuwa katika ngazi
ya Mabalozi.
Wakizungumza
mara baada ya utiaji sahihi hati hizo,
wawakilishi hao wameelezea kuwa
kuanzishwa kwa uhusiano huo ni hatua
muhimu sana katika kukuza na kuendeleza
ushirikiano na uhusiano kati ya mataifa
hayo mawili na watu wake.
Tanzania imekuwa ikinufaika kwa ufadhili wa nafasi za
masomo kutoka Malta kwa watumishi mbalimbali wakiwamo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara nyingine.
No comments:
Post a Comment