SHEHA wa shehia ya Utaani wilaya ya wete Pemba, nd: Massoud
Msellem Shinei, akifungua mkutano wa kuelimishwa namna ya kuandikwa sheria na
mafunzo ya katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, ZLSC
tawi la Pemba, uliofanyika skuli ya Chasasa sekondari wilayani humo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
KAIMU Mratibu wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar, ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed akielezea kazi na
majukumu ya kituo hicho, kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuelezwa wananchi namna
ya kuandika sheria na mafunzo ya katiba,uliofanyika skuli ya Chasasa wilaya ya
Wete, kulia ni mwanasheria wa serikali Ali Amour na kushoto ni sheha wa shehia
ya Utaani, Massoud Msellem, akifuatiwa na Afisa Mipango wa ZLSC Siti Habib Mohamed,
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
MCHANGIA mada, akiuliza suali lake la kutaka tofauti kati
ya katiba na sheria, kwenye mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba juu ya kuwaeleza wananchi taratibu za kuandika
sheria na mafunzo ya katiba, mkutano huo ulifanyika skuli ya Chasasa wete
Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
SHEHA wa shehia ya Majenzi wilaya ya
Micheweni Pemba Faki Kombo Hamad, akifungua mkutano wa elimu ya katiba na
utaratibu wa kuandikwa kwa sheria, mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, kulia ni Mratibu wa kituo hicho Fatma
Khamis Hemed na kushoto ni mwanasheria Omar Ahmed Abdalla, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
BAADHI ya wananchi wa wilaya ya Micheweni
wakifuatilia kwa makini mada ya utaratibu wa uandishi wa sheria, kwenye mkutano
maalumu uliofanyika skuli ya Micheweni, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar, ZLSC tawi la Pemba, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment