Habari za Punde

Mafunzo ya kuwakumbusha wasaidizi wa sheria na masheha kisiwani Pemba sheria mpya,

 MRATIBU wa mafunzo ya kuwakumbusha wasaidizi wa sheria na Masheha kisiwani Pemba sheria mpya, Safia Saleh Sultan, akielezea juu ya mafunzo hayo, yaliofanyika mjini Chake chake, kulia ni Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi Pemba, Fatma Khamis Hemed na katikati ni Katibu Tawala wilaya ya Chake chake Rashid Hadid Rashid, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
 KATIBU Tawala wilaya ya Chake chake Rashid Hadid Rashid akifungua mafunzo ya kuwakumbusha wasaidizi wa sheria na masheha kisiwani Pemba sheria mpya, mafunzo hayo yaliofanyika mjini Chake chake, yameandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni Mratibu wa ZLSC Fatma Khamis Hemed na kushoto ni Afisa Mratibu wa mafunzo hayo Safia Salehe Sultan, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MSAIDIZI wa sheria kutoka JKU Pemba, Jaffar Abdalla Ali akichangia mada, kwenye mafunzo yaliowashirikisha wao na masheha juu ya ujio wa sheria mpya, mafunzo yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika mjini Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WASHIRIKI wa mafunzo ya kutambulisha sheria mpya za Zanzibar, ambao ni wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Pemba pamoja na baadhi ya masheha wakisikiliza mada iliowasilisha na Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed hayupo pichani, mafunzo hayo yamefanyika mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba)  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.