Habari za Punde

Taarifa ya Ofisi ya Makamo wa Rais kuhusu uzushi kwenye mitandao ya kijamii



Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Habari hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.


Aidha tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.

Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa
Makamu wa Rais
10/8/2015

1 comment:

  1. kwa kweli, hali ya siasa nchini sio nzuri sana hasa ktk chama cha mapinduzi kufuatia mchakato wa kumpata mgombea urais nadani ya chama hicho, pamoja na matukio yaliofuatia mchakato huo.

    La kusikitisha zaidi ni kwamba hatujapata tamko rasmi na la maana kutoka CCM wakati uharibifu ukizidi kufanyika NDANI YA CHAMA ktoka kwa wale ambao"mchana CCM usiku UKAWA, hasa huku Bara!

    Kwa mfano taarifa hii ya Dr. Bilali, kwanini mitandao husika isichukuliwe hatua wakati ni juzi tu, bunge lilipitisha sheria ya makosa ya mitandao na Rais ameshaisaini? na mtandao wenyewe ni JAMII FORUM mitandao mingnine yote imekopi kutoka Jf?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.