Habari za Punde

Mhadhiri na Mwalimu Yussuf Shoka Hamad alipozungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu huria ( Open University)




Mhadhiri wa chuo kikuu cha Cambridge cha Marekani,Yussuf Shoka Hamad, akizungumza na wanafunzi wa Open University katika mdahalo wa wazi uliofanyika ukumbi wa Suza Pemba  juu ya Changamoto inazozikabili Changamoto Sekta ya Elimu ya juu Tanzania.

 Mkurugenzi wa Chuo kikuu huria Pemba, Juma Rashid Khamis, akielezea umuhimu wa mjadala wa wazikwa Wanafunzi wa Vyuo vikuu  kwa Wanafunzi wa Chuo hicho Tawi la Pemba
 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo kikuu Huria Tawi la Pemba, wakimskiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kamrige cha Marekani , Yussuf  Shoka Hamad , wakati akiwasilisha katika Mjadala wa Wazi kwa Wanachuo wa  Chuo Kikuu Huria Pemba, juu ya Changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu ya juu Tanzania, uliofanyika huko katika ukumbi wa SUZA Pemba.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo kikuu Huria Tawi la Pemba, wakimskiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kamrige cha Marekani , Yussuf  Shoka Hamad , wakati akiwasilisha katika Mjadala wa Wazi kwa Wanachuo wa  Chuo Kikuu Huria Pemba, juu ya Changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu ya juu Tanzania, uliofanyika huko katika ukumbi wa SUZA Pemba.

Picha na Bakar Mussa .Pemba

8 comments:

  1. Assalamu Alaykum ! Kazi nzuri mhadhiri na mwalimu wa chuo kikuu kwa kuongelea maswala ya Elimu ya huko Pemba na Zanzibar kwa ujumla! Naomba nichangie tu kuwa hichi chuo kikuu cha Cambridge kipo nchini Uengereza na sio Marekani kama invyoonekana hapo juu! Shukran

    ReplyDelete
  2. Jamani, wakati sasa umefika tubadilike kidogo, hivi kweli huyo aliesimama ndie MKURUGENZI wa tawi la chuo kikuu huria Pemba?...MKURUGENZI?..nadhani mpiga picha atakua amejichanganya!

    Kama kweli ni mkurugenzi, basi anahitaji kua 'smart' kidogo ili aitendee haki elimu yake, elimu jamani inakwenda na utamaduni wake, kama ni ya Dini au ya magharibi!

    Kwa muda mrefu sasa Z'bar tumeshindwa kuliona jambo hili na mtu ukimwambia anakimbilia UISLAMU au UTAMADUNI...jambo ambalo ni kisingizio tu!

    Halafu unakuta mtu kama huyo anatamani apewe nafasi ya UBALOZI wa jamuhuri kwasababu tu ana "masters degree"...msiba mkubwa huu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau umetoa point lakini bado hujatusaidia sana. Huo u-smart ulikusudia uwe vipi? Avae tai, anyoe ndevu, avae suti au hasa ungetusaidia kidogo. Halafu umesema watu ukiwaambia wanakimbilia uislamu au utamaduni, suali linakuja kwani uislamu ndio unaohimiza watu kutokuwa smart? Kama ndio kivipi. Ungesaidia sana jamii kama unge-define u-smart uliokusudia.

      Delete
  3. 'u-smati hapa nimekusudia ; mavazi, 'posture' (namna ya kusimama na kuwaangalia watu) unapohutubia, pamoja na unadhifu wa kuchonga ndevu!

    Naelewa, mkakati hapo ni kumtetea lkn. naamini jamii hii haiwezi kupiga hatua kama tutaendelea kutokukusoana na kulea 'ujinga'

    Mimi naelewa Z'bar tumekua wagumu mno kubadilika ktk baadhi ya mambo hususana mavazi, utamkuta mbunge amevaa suti na kofia kama vile MREMA kisingizio Uislamu na Utamaduni lkn. ikifika wakhti wa salaa wenzake wanatoka yeye anabaki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Mrema anavaa kofia kwasababu ya Uislamu? Amewahi kusema mwenyewe au vipi. Jee hakuna watu wa bara ambao si Waislamu wanaovaa kofia. Mimi nafikiri kofia ni vazi la waswahili pia kama ilivyo kanga.

      Delete
    2. Mdau bado khasa hujatwambia usmati ni nini kama ni posture wewe umeangalia picha moja tu na kutoa hukumu kama ndevu Naona zimechongwa vizuri tu. Kama ni suti nani kakwambia lazima uvae suti ndio tuwe smart? Yaani LAziMA tuige hata mavazi ndio tuwe smart?? Hatujithamini name hatuthamini vyetu. Hivi lazima tuige hats mavazi ndio tuwe tumeendelea? Yapo ya kuiga lakini sio kila kitu. Yawezakana we we no mpenda suti sio mbaya, yawezekana sio miongoni mwa wafuga ndevu sio mbaya lakini isiwe sababu ya kuwafanya watu wajinga eti kwa sababu tu hawapendi Yale unayoyapenda wewe.

      Delete
  4. Huyu Sh Yussuf ni mhadhiri cambridge au ni mwalimu wa Kiswahili? Naona kwenye website imeandikwa Yussuf Hamad
    Position:

    CULP Swahili Teacher
    Contact Information

    Email: yh360@cam.ac.uk
    Mimi kumbukumbu zangu Sh Yussuf ni mhadhiri chuo kikuu cha SOAS. Naomba nisahihishwe kama nimekosea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yeye si mhadhiri wala hawezi kuwa mhadhiri kwa sababu hana digrii. Ni lector, siyo lecturer. Yaani mwalimu wa Kiswahili.

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.