Habari za Punde

Ujumbe kutoka Sweden wawasili kuendelea mahusiano na wadi za Makunduchi

 Wadi za Makunduchi zimejipanga kuitikia wito wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein katika vita dhidi ya unyanyasaji wa wanawake na watoto kwa kushirikiana na Manispa ya Kiruna, Sweden. 

Kikosi cha vita hivyo kutoka Kiruna kikiongozwa na bi Jenny Lindberg  (Hayupo kwenye picha) kimewasili Zanzibar kwa ajili ya matayarisho ya mradi wa kupambana na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto unaotegemewa kuanza karibuni. 

Katika picha anaonekana bi Eva Raattamaa, muuguzi na mkunga akifuatiwa na afisa wa polisi anayeshughulikia upelelezi wa makosa ya jinai Ulrika Larsson aliyevaa miwani nyeusi na bi Gunborg Flygare ambaye ni "social worker" Kwenye uwanja wa ndege ujumbe huo umepokelewa na bi. Mwatima Hassan mwenye mtandio mwekundu, Jaku na Mohamed Muombwa (hawapo kwenye picha)



Ujumbe kutoka Kiruna, Sweden upo nchini kwa mazungumzo ya kuendeleza uhusiano kati ya wadi za Makunduchi na Manispa ya Kiruna. Ujumbe huo umekutana na kamati ya wadi za Makunduchi huko hoteli ya Madrugada  kigaeni Makunduchi. 

Miongoni mwa masuala yaliyokubaliwa ni kuendelea kwa mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana wa Makunduchi pamoja na kuanzisha uhusiano kati ya skuli za Kiruna na Makunduchi. Ujumbe wa Makunduchi uliongozwa na ndugu Mohamed Muombwa (hayupo kwenye picha) na ule wa Kiruna uliongozwa na ndugu Ove wa pili kutoka kushoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.