Habari za Punde

Dk. Shein Arejesha Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Afisi za Tume Bwawani Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai alipowasili Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zuilioko katika Hoteli ya Bwawani Zanzibar akirejesha faomu ya kugombea Urais Zanzibar. , 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi wa CCM alipofika kurejesha fomu  za kugombea Urais  wa Zanzibar kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipowasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa ajili ya kurejesha fomu za kugombea Urais wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe,Jecha Salim Jecha (aliyesimama) akimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuweza kukamilisha taratibu zote za ujazaji wa Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar wakati aliporejesha fomu hizo leo katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja,(kulia) Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (NEC) Ng,Salim Kassim Ali,wakiwepo na wajumbe wa Tume hiyo


Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi walioshuhudia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein ,akirejesha fomu  za kugombea Urais  wa Zanzibar kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe,Jecha Salim Jecha  katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja leo
Baadhi ya Viongozi wa CCM Zanzibar wakifuatilia hafla ya kurejesha Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, leo asubuhi Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akionesha mkoba wa fomu za Urais wa Zanzibar wakati akirejesha Fomu hizo Afisi ya Tumu ya Uchaguzi Zanzibar zilioka katika hoteli ya bwawani Zanzibar. leo asubuhi.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi fedha tasilim Shilingi za Kitanzania Millioni mbili Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe,Jecha Salim Jecha wakati  aliporejesha fomu  za kugombea Urais  wa Zanzibar   katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja leo













No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.