Habari za Punde

Maziko ya Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana leo

  WAUMINI mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, wakimswalia Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, swala iliyofanyika huko kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Ksiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)

 WANANCHI mbali mbali Kisiwani Pemba wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, kuupeleka kwenye makaazi yake ya Mwisho huko kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akishuhudia mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, Mhe:Jabu Khamis Mbwana marehemu alifariki dunia jana na kuzikwa huko kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akitia mchanga kwenye kaburi la Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, aliyefariki duania jana na kuzikwa kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akiitikia dua mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, aliyefariki dunia jana na kuzikwa kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akikabidhi ubani kwa mmoja wa vizuka wa marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, aliyefariki dunia na kuzikwa kijijini kwao kiuyu Mbuyuni Kisiwani Pemba. .(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.