
Marehemu Jabu Khamis Mbwana alikuwa akisumbuliwa na homa kwa takriban wiki moja iliyopita.
Umati Mkubwa wa Wananchi, waumini wa Dini ya Kiislamu, Viongozi wa Kiserikali pamoja na Vyama vya Siasa wakijumuika pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walihudhuria mazishi ya
Kiongozi huyo aliyekuwa na Fani ya Tasnia ya Habari.
Marehemu Jabu Khamis Mbwana alizaliwa mwaka 1958 na kupata elimu ya msingi katika skuli ya Kiuyu Mbuyuni na baadaye elimu ya Sekondari katika Skuli ya Fidel Castrol Chake chake Pemba.
Alijiunga na mafunzo ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Habari Tanzania { TSJ } na kupata Stashahada ya fani hiyo mwaka 1984 ambapo aliajiriwa kazi ya Afisa wa Habari Wilaya ya Micheweni.
Marehemu Jabu KhaMIS Mbwana Aliamua kuingia katika ulingo wa Siasa na kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Vipindi viwili kuanzia kwamba 1985 hadi mwaka 1995.
Utumishi wake makini uliozingatia maadili na nidhamu kwa Jamii ulimuwezesha kuteuliwa kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba mwaka 1996.
Mwaka 2006 Marehemu Jabu Khamis Mbwana aliteuliwa na Rais wa Zanzibar kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake chake, Wilaya ya Mkoani na hadi kufariki kwake alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni.
Nd. Jabu alikuwa Mfanyakazi hodari, shupavu, aliyejiamini katika utumishi wake na mwenye mashirikiano na watendaji wenzake wa Serikali na alimthamini kila mtu katika Uongozi wake.
Akiwasilisha salamu za Rais wa Zanzibar kwenye maziko hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Dr. Ali Mohammed Shein amepokea kwa mshituko taarifa ya Kifo cha Msaidizi wake
katika Wilaya ya Micheweni Nd. Jabu Khamis Mbwana.
Alisema kifo hicho hakikuacha pengo wala msiba kwa familia pekee bali kwa Taifa zima jamii ikikumbuka ushupavu wa ndugu Jabu wakati wa uhai wake katika kusimamia haki na uadilifu.
Balozi Seif aliyepokea simu kutoka kwa Rais wa Zanzibar muda huo wa mazishi aliitaka familia ya marehemu pamoja na marafiki kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kifupi cha msiba.au kukinga jambo hilo. Na hivyo ndivyo wajibu huo ulivyomkuta Ndugu Jabu Khamis Mbwana.
Mauti yanakata starehe ya Dunia, hayana kinga na kamwe hayazoeleki jambo linaloiwajibikia kila nafsi kujiandaa na haki hiyo.
Marehemu Jabu Khamis Mbwana ameacha familia ya vizuka Watatu na watoto 17. Mwenyezi Muungu ampe safari njema Marehemu Jabu. Amin.
No comments:
Post a Comment