Habari za Punde

Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar atowa maelezo ya kuchelewa kulipwa Penshini

Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar Ndg Justin,S.Nandonde akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na malalamiko ya Wateja wao askari waastafu kwa kuchelewa kulipwa pensheni zao kupitia katika akaunti zao. 

Tatizo hilo limetokana na malipo yao kupelekwa katika benki ya PBZ kutoka hazina Dar na kusababisha sintofahamu hiyo ya kuchelewa kulipwa pensheni yao na kusema tatizo hilo linashughulikiwa kwa kuwasiliana na hazina Dar es Salaam ili kuweza kutiliwa pensheni zao na kulipwa kwa wakati. 

Amesema tatizo hilo limejitokeza kutokana na wateja wao mwanzo walikuwa wakitumia benki ya PBZ, ndio ikasababisha kupelekwa huko. kabla ya kujiunga na benki ya posta.

1 comment:

  1. Kwa Tz ni jambo la kawaida tu Hilo na kama sababu hizo hazitoshi mloletewa basi tutakuleteeni nyengine.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.