STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Pemba 2.10.2015

WANANCHI kisiwani Pemba wametakiwa kuwachagua viongozi wa CCM ambao watakaa
pamoja na wao na sio wale viongozi wanaowachagua kutoka vyama vya upinzani ambao
wakishapata nafasi za uongozi huwakimbia na kutojali matatizo yao.
Hayo yalielezwa leo na baadhi ya Viongozi
wa CCM Zanzibar, katika Mkutano wa
Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliofanyika katika Jimbo la Gando, Mkoa wa Kaskazini Pemba uliohudhuria na
maelfu ya wanaCCM na wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa mgombea Urais wa
Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein.
Viongozi hao walieleza kuwa viongozi wa
vyama vya upinzani wanaochaguliwa na wananchi kisiwani Pemba mara baada ya
kupata nafasi za uongozi huhamisha makaazi yao kisiwani humo na kuwasahau
waliowachagua.
Katika mkutano huo Balozi Seif alisema
kuwa amekuwa akipata amaelezo kutoka kwa wanachama wa CUF kuwa hivi sasa
wamechoka kudanganywa na kuwaambia kuwa umefika wakati wa wao kujiunga na CCM.
"CUF imekuwa sawa na timu ya mpira
kila siku ikiingia uwanjani inapigwa mabao hiyo si timu kwa nini wewe ubaki
huko njooni CCM Sera zake zinatekelezeka tizameni ndani ya miaka mitano
ilivyofanya... na karibu tunatengeneza barabara ya Wete- Chake"alisema
Balozi.
Alisema kuwa Dk. Ali Mohamed Shein
amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi ya kununua meli mpaa
ambayo itaingia nchi wakati wowote na Dk. Shein ndie atakae izindua.
Aidha, alisema kuwa CCM haitaki fujo wala
shari huku akishangwaza na mgombea urais wa CUF ambaye ameanza kugombea nafasi
hiyo tokea ujana wake.
Aliwataka wananchi kujiunga na CCM kwani
ni chama ambacho hakijawahi kushindwa.
Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu
Ameir Kificho alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miundombinu ya barabara Pemba
imeimarika na kutoa shukurani kwa Dk. Shein kwa maendeleo yaliopatikana kisiwa
humo.
Kificho alisema kuwa Zanzibar imeimarika
kutokana na amani iliyopo hatua ambayo imepelekea kukua kwa sekta za maendeleo
ikiwemo sekta ya utalii.
Aidha, alisema kuwa chama vyama vya
upinzani vimekuwa havina hoja kutokana na maendeleo makubwa yaliofikiwa
kisiwani humo na ndio maana vimekuwa
havizungumzii kuhusu maji, barabara, umeme, afya, elimu na sekta
nyenginezo hiyo ni kutokana na kuwa vyote hivyo vimetekelezwa na Serikali ya
CCM.
Alieleza kuwa kinachofanywa na vyama
hivyo hivi sasa ni kudandia hoja ambazo tayari zimekuwa zikifanyiwa kazi na
Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM chini ya uongozi wa Dk. Shein huku
akieleza haja ya Dk. Shein kupewa kura za ndio ili maendeleo zaidi yaweze
kupatikana Unguja na Pemba.
Aliwataka wananchi hao wa Pemba
kutowachagua viongozi ambao mchezo wao ni kukimbia katika vyombo vya kutunga
sheria kama walivyofanya katika Baraza la Wawakilishi, Bunge la Katiba na Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nae Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai
Nahodha aliwaomba wananchi wa Pemba kujua kuwa viongozi waa CUF wameshindwa
kufanya kazi za siasa na kuwaauliza viongozi wa chama hicho hata kujenga
madarasa wanasubiri mamlaka kamili.
Aliwataka wananchi wa kisiwa cha Pemba
kufanya mabadiliko na kuwachagua viongozi wa CCM kwani viongozi wote
waliowachagua katika uchaguzi uliopita wakiwemo Wawakilikishi, Wabunge na
Madiwani wa CUF wameshindwa kuwatumikia wananchi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na
Waziri wa Maji, Ardhi na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban alisema kuwa iwapo wananchi watamchagua Dk.
Shein suala la mafuta na gesi litafanyiwa kazi vizuri kutokana na juhudi zake
alizokwisha kuzianza.
Alisema kuwa suala la mafuta na gesi
halikuanza leo kwa sababu watu ya kupiga kuwa kwani suala hilo limeanza tokea
mwaka 1951 na Serikali iliyoopo amdarakanai inaendelea.
Alisema kuwa tokea alipoingia madarakani
kuwa Waziri wa Wizara hiyo tayari Dk. Shein ameshaweka nguvu kubwa katika
kuiendeleza sekta hiyo kwa ziara mbali mbali duniani na hadi leo amekuwa
akiihangaikia kazi hiyo na anaiweza.
Aliwataka wananchi kutodanganyika kwani
mafuta na gesi hayachimbwi kwa siku mia moja kama wanavyoelezwa na viongozi wa chama
cha CUF.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Vuai Ali Vuai aliwapongeza wananchi wa Pemba kwa kuhudhuria kwa wingi katika
mikutano ya Kampeni za CCM na kuomba kwamba kutokana na kiu ya wananchi kutaka
kuirimbua meli mpya inayotarajiwa kuwasili hivi karibuni iwachukue bure
wananchi wa Pemba na akuwapeleka Unguja kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dk.
Shein.
Alisema kuwa CCM mara hii itahakikisha
inapata Majimbo yote ya Zanzibar na kuwaomba wazee, vijana pamoja na makundi
yote kumchagua Dk. Shein kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuleta maendeleo na
kuweza kuwaunganisha wananchi.
Sambamba na hayo, Vuai alisema kuwa Dk.
Shein ni kiongozi wa watu kwani hana ubaguzi, hana choyo wala hana makuu pia,
ni kiongozi ambaye anasimamia Katiba ya nchi bi la kumuogopa mtu yoyote.
Bi Zainab alisema kuwa katika uchaguzi wa
mwaka huu wanaCCM wa Pemba wanatakiwa kushinda kwa kishindo na kupata viti
kupitia wagombea wake.
Nae Bi Modlin Kastiko alisema kuwa kuna
kila sababu ya kumchagua Dk. Shein kutokana na juhudi zake kubwa za kuimaarisha
sekta za maendeleo ambazo zimeimarika
kwa upande wa Unguja na Pemba zikiwemo miundombinu ya barabara, elimu, afya,
maji, umeme na nyenginezo.
Alisema kuwa hivi sasa kumekuwa
kukitokezea vitisho vya kila aina na tayari wapo wanaCCM waliochomewa moto
nyumba zao kwa sababu ya kukataa kutoa kadi zao za kupigia kura kisiwani humo.
Kastiko aliwataka akina mama, vijana
pamoja na wananchi wote wa Pemba wasikubali kutishwa licha ya vitimbi vinavyoendelea kufanywa na wafuasi wa
vyama vya upinzani huku akiwataka kuwapigia kura viongozi wa CCM ili kuimarisha
amani na utulivu.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment