Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakijitokeza kwa Wingi kufuatilia mazoezi ya Timu yao inayojiandaa ni Michuano ya Kombe la Chalenji yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huo Nchini Ethiopia. wakiwa katika uwanja wa Amaan wakifuatilia mchezo wao wa tatu wa mechi za kirafiki kujiandaa ni michuano hiyo katika mchezo huo imeshinda bao 1--0.
Benchi la Jopo la Wachezaji na Makocha wakifuatilia mchezo wa kirafiki wa timu yao uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Taifa ya Zanzibar ikiwa katika michezo yake ya kujiandaa na michuano hiyo ya Kombe la Chalenji.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar akimpita Beki wa Timu ya Wachezaji Bora wa Kombe la Makocha Zanzibar, katika mchezo wa kujipima nguvu ikiwa ni mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na Michuano ya Chalenji Nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huo.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Malale Hamsini akitowa maelekezo kwa mchezaji wake Mateo Antony wakati wa mchezo wa kirafiki wa timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Ethiopia mwezi huu. Michuano hiyo inatarajiwa kuaza tarehi 21 Novemba kwa mchezo ya Ufunguzi kati ya Timu ya Taifa ya Zanzibar na Uganda.
Mchezaji timu ya Kombaini ya Wachezaji Bora wa Kombe la Makocha Zanzibar akiwa na mpira huku beki wa timu ya Taifa ya Zanzibar wakiwania mpira huo wakati wa mchezo wao wa kirafiki kuipa mazoezi timu ya Taifa ya Zanzibar inayojiandaa na Michuano ya Chalenji inayotarajiwa kufanyika Nchini Ethiopia mwezi huu.
Mchechaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar Selembe, akiwa na mchezaji wa timu ya Kombaini ya Wachezaji Bora wa Kombe la Makocha Zanzibar katika mchezo wa Kirafiki uliofanyika uwanja wa Amani Zanzibar, Timu ya Taifa ya Zanzibar imeshinda Bao moja kwa njia ya penenti.
Wapenzi wa mchezo wa Mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa Kirafikin wa Timuyao ya Taifa ya Zanzibar uliofanyika katikas uwanja wa Amaan Zanzibar kati yao na timu ya Kombaini ya Wachezaji wa Michuano ya Kombe la Makocha Zanzibar katika mchezo huo Timu ya Taifa ya Zanzibar imeshinda bao moja.
No comments:
Post a Comment