Na Mwandishi wetu, Pemba
OKTOBA 28, mwaka 2015 Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Jecha Salim Jecha, alitangaaza rasmi kuyafuta
matokeo ya uchaguzi mkuu ngazi ya udiwani, uwakilishi na urais wa Zanzibar.
Kila
mmoja ni shahidi wa hili, na wala sina nia ya kukumbushia pakubwa, maana wapo
waliofurahia wakiwa na sababu kadhaa, lakini pia wengine walinuna nao wakiwa na
sababu tunasema zenye akili.
Yote
kwa yote ndio tumeshashuhudia kwamba matokeo hayo yamefutwa, na mfutaji akiwa
na sababu kadhaa, ikiwemo uchaguzi huo kutawaliwa na ghilba.
Kisha
ufutaji huo ukasindikizwa kisheria zaidi kwa taarifa hiyo, kuingizwa kwenye
gazeti rasmi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wengine kufikiria kwamba ni Gazeti
la Zanzibar leo, kumbe silo hili ni maalum hilo.
Niende
mbele kwanini uchaguzi ulifutwa……hapana kila mmoja anaelewa sababu kadhaa, na
kisha Mwenyekiti wa ZEC kutangaza kwamba uchaguzi huo, utarejewa na vyama
kuingia tena dimbani.
Wala
sio siri…. na wala sioni aibu kusema kuwa Chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF
walishatangaaza mara kwa mara na kwa hati nyeusi kwamba, wao hawafahumu kufutwa
huko na wala hawana habari na uchaguzi wa marejeo.
Huku
chama kinachotetea kiti chake cha utawala cha CCM kwanza kikikubaliana na
ufutwaji huo, na kisha kimeshajipanga ili kuingia tena kwenye marejeo ya
uchaguzi huo.
Na
hii ndio demokrasia, kwamba mmoja akisema hii nguo ni nyeusi, basi atokea
mwengine aseme sio nyeusi, bali ina
rangi tu nyeusi, lakini wote wanasema hayo sio kwa utashi bali kwa nguvu ya hoja
tena nzito.
Kama
ZEC ilishatangaaza kwamba kuna uhakika wa kurejea kwa uchaguzi, akina mimi na
yule tumekuwa tukisema kila mara kwamba, lazima amani na utulivu katika
uchaguzi huo, ipigie chapuo.
Walishasema
wazee kwamba ‘hakuna harusi ndogo wala isio na gharama, basi tusema kwa pamoja
kwamba, na lolote kwenye uchaguzi laweza kujichomoza.
Wiki
tatu kabla ya uchaguzi wa mwanzo Oktoba 25 mwaka 2015, viongozi wa dini zote
unazozijua wewe, makababila, vyama vya siasa, wanawake, vijana na mashirika
kadhaa yalismama na kuomba amani na utulivu hadi nykati za usiku.
Sasa
tumekwama wapi kwa uchaguzi huu ambao vyombo vyenye mamlaka vinasimama na
kusema utarejewa, na kauli za hivi karibuni kwamba ni mwezi wa Januari 2016 au
hata kabla ya kumalizika kwa mwezi wa Febuari.
Nakumbuka
sana mikutano yote ya kamapeni iliofanywa kabla ya kuhitimishwa pale oktoba 24
mwaka 2015, hakuna kiongozi wa chama cha siasa, ambae hakuna neneo amani na
utulivu kwenye hutba yake.
Kumbe
kila mmoja aliona umuhimu wa kudumisha na kuendelea amani na utulivu, tena
kabla, wakati na baada ya uchgauzi, tukiamini kuwa kumbe bila ya vitu hivyo
hakuna linalofanyika.
Mgombea
urais wa chama cha CUF maalim Seif Sharif Hamad kwenye mkutano wake wa kampeni alioufanya
katikati ya kijiji alichozaliwa cha Mtambwe, alisisitiza umuhimu wa amani na
utulivu.
“Ndugu
wananchi nasema Jeshi la Polisi sasa limeshatufahamu sisi CUF nini lengo letu,
sasa lazima tuhakikishe tunatunza amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu’’,alisema.
Kwani
alikuwa yeye tu….. hata Mgombea wa nafasi kama hiyo kutoka AFP Said Soud Said,
yeye alisema lazima kila mmoja neno amani na utulivu liwe mbele kisha ndio
chama.
Alikwenda
mbali zaidi kwamba, hakuna umuhimu wa uwepo wa chama chochote Zanzibar, kwamba hakitozingatia
amani kwa wananchi, maana urais, umakamu na uwaziri hautafanyika kama amani
haitotawala.
Lakini
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati akimuombea kura mgombea
wa chama hicho Dk Ali Mohamed Shein, kwenye mkutano uliofanyika Kiwani, alisema
chama hicho hakijapanga vijana kufanya fujo.
“CCM
ni mwalimu wa demokrasia, CCM ndio chama mama, hakina haja ya kuvunja amani,
maana chenyewe kinatetea amani na utulivu’’,alisisitiza.
Sasa
iwe wewe unaeshiriki au uko kando kwenye uchaguzi wa marejeo, ni vyema suala la
amani na utulivu likapigiwa chapuo, maana hakuna asietaka utulivu na anaewania
fujo.
Kama
vyombo vyenye mamlaka vimeshasema uchaguzi unarejewam mbona hatuoni shamra
shamra za hutuba za viongozi wa dini na vyama vya siasa kusimama kidedea juu ya
amani na utulivu.
Maana
hapa narejea tena iwe wewe ni mshiriki wa uchaguzi au wa kukaa kando, lakini je
amani na utulivu huna shida navyo tena, naamini jawabu sio, sasa tuipige
chapuo.
Kijana
Omar Kombo Daudi (22) wa Mkoani, anasema chakuhubiri
kwa sasa kama mamlaka
zimeshamua kurejea uchaguzi, ni amani na utulivu maana bado wananchi wanahitaji
hilo milele.
“Hakuna
hata kiongozi mmoja wa dini, chama, au NGOs na wengine asietaka amani na
uutulivu, sasa lazima tuone yale maombi kadhaa yaliofanywa
yarejewe’’,alifafanua.
Bibi
Asha Hassan Makame (50) wa Chakechake, anasema lazima kila mmoja apigie chapuo
suala la amani na utulivu, maana hakuna
uchaguzi uliohakikishiwia amani na utulivu kwa asilimia mia moja.
“Inawezekana
kuna vyama havitoshiriki uchaguzi wa marejeo, lakini bado vinastahili kuomba
amani na utulivu, maana hata wao watakaobakia majumbani wanahitaji
amani’’,alisema.
Ingawa
Mwanaidi Mbarawa Hija (35) anasema suala la amani na utulivu sio tu kwenye
mambo ya kisiasa pekee, bali hata wakati wowote kila mmoja aombe amani na
utulivu.
“Unajua
suala la amani ni wakati wote, lakini kama kuna shughuli za kisiasa kama
uchaguzi, lazima kila kiongozi kwa nafasi yake akemee, maana amani ni kwa sote
na machafuko pia’’,aliweka wazi.
Bado
upo umuhimu kwa kila mmoja, iwe wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa marejeo au
hata katika maisha ya kila siku, suala la amani na utulivu pia ni sehemu ya
maisha.
Yote kwa yote suala la amani na utulivu,
ambalo dini zote inalikubali lazima kwa Zanzibar kuelekea uchgauzi wa marejeo
iwe ndio ajenda kuu, maana athari na faida ni kwa wote.
Mimi si mwanachama wa chama chochote, ila ni mpigania maendeleo katika visiwa vyetu, napenda sana kuona kiongozi mwenye kuleta amani na maendeleo ya kweli katika nchi yake.
ReplyDeleteNilikuwa mfatiliaji mzuri tangu vyama vyote vilivyoanza kampeni hadi siku ya Uchaguzi, lakini kwa mtazamo wangu wa kawaida nahisi CCM Zanzibar hawapo tayari kwa demokrasia ya kweli.
Naamini hata wapinzani wakiweza kutawala nchi haitokuwa na machafuko kwani wazanzibari ni watu wenye kupenda amani na utulivu.
CCM zanzibar lazima wakubali matakwa ya wananchi wakubali kuwa wazanzibari sasa wanataka kuona mabadiliko katika nchi yao, naamini hata wapinzani hawataweza kuleta maendeleo ya mara moja lakini mabadiliko yanahitajika Zanzibar, Miaka zaidi ya 40 ya CCM ni kipimo kikubwa kama ni chama cha kuleta maendeleo, sasa imefika muda wa wapinzani kuongoza Zanzibar alau kwa miaka5 iwe Chadea, iwe Chauma iwe JahaziAsilia au hata Cuf.
Mabadiliko yanahitajika Zanzibar hata Muandishi unalijua hilo kwani katika wakati wa kampeni uliweka katika Blog yako kura za maoni ni ushahidi tosha kuwa waZanzibari wanataka mabadiliko ya kweli kwa njia ya AMANI NA UPENDO.