Habari za Punde

Fedha, Mkesha wa Amani Kuokoai Vifo vya Wajawazito na Watoto

Na  Skolastika Tweneshe-Maelezo

Fedha zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea 

amani  nchini zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji  hasa 

afya ya mama na mtoto.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu  Godfrey  Malassy  alipokuwa 
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Malassy alisema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha 

hilo zitanunua vifaa vinavyotumia nishati ya jua (solar Panels) ili 

kuwasaidi wamama wajawazito na watoto wanaozaliwa.

“Kina mama wajawazito na watoto wanakufa mahospitalini 

kutokana  na kukosa umeme hasa vijijini,  hivyo tumeamua fedha 

zitakazopatikana mkesha huu tutanunua solar” alisema Malassy

Aidha Askofu Malassy  amewaomba wananchi   kuzidi 

kumuombea Rais John Magufuli katika kuliongoza Taifa la 

Tanzania ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi ambayo tayari 

imekubalika ndani na nje ya nchi.  


Mwenyekiti huyo alitambulisha kitabu  kiitwacho IJUE  SIRI YA 

AMANI  KWA  TAIFA ambacho  kinauzwa Sh.5000 amesema 

kuwa  kitabu hicho kina lengo la kuelimisha thamani na jukumu la 

watanzania kuilinda Amani  bila kujali itikadi za  dini, siasa wala 

ukabila

Pia ameomba kwa atakaeguswa na  matatizo yanayowakumba 

wamama wajawazito anaweza kutuma mchango wake kwa namba 

zifuatazo 0755202204,0719202204,0684202204.

Mkesha huo  ni wa 18 tangu uanze kufanyika  na mwaka huu 

utafanyika  katika Uwanja wa Uhuru usiku wa tarehe 31 ambapo 

mgeni rasmi atakuwa Rais wa Awamu ya Tano Mhe.  John Pombe 

Magufuli.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.