Habari za Punde

Makaburi ya Mwanakwerekwe yalianza kutumika kuzikia tokea 1965


 Baadhi ya makaburi yaliopo Mwanakwerekwe hii ni sehemu muhimu ya kukumbushana mauti kwani Mtume Swalla Allaahu 'alayhi Wasallam alituusia sana tukumbuke sana kile kinachoondosha na kuvunja ladha akikusudia mauti.

 Baadhi ya makaburi yaliopo Mwanakwerekwe sehemu ambayo ilianza kutumika kwa kuzikia tokea mwaka 1965 na kwa mujibu wa wasimamizi wa sehemu hii bado ina nafasi ya kutosha kuendelea kuzika maiti zetu.
 Wakati ukiingia sehemu ya makaburi ya Mwanakwerekwe unakutana na ujumbe huu huu muhimu ambao ni dua iliyosuniwa kusomwa wakati wa kufanya ziara makaburini. Kila mwenye kutembelea makaburi iwe ya jamaa zake au ya mtu yeyote ni Sunna kuisoma dua hii. Ipo haja kwa wasimamizi wa sehemu hii kulifanyia ukarabati bango hili 
 Wakati nilipofanya ziara ya kutembelea makaburi ya Mwanakwerekwe nilikutana na msimamizi mmoja ambae anafanya kazi ya kuchimba makaburi katika sehemu hii tokea mwaka 1995. Msimamizi huyu alinishangaza kwa uzoefu wake kwani kila nikimtaja mmoja wa jamaa zangu na kuulizia wapi lilipo kaburi lako alinipeleka moja kwa moja kaburini hapo bila ya kukosea. Amenipa somo moja kubwa sana kuhusiana na uzoefu wae wa kuweka kumbukumbu kichwani kwa uhakika.
Mlango mkuu wa kuingilia sehemu ya makaburi ya Mwanakwerekwe ambayo ni safari ya mwisho ya kila aliyejaaliwa uhai atapaswa kuikabili.

3 comments:

  1. Mola awarehem maiti wetu waliotangulia mbele ya haki awasamehe kwa yote waliyokosea Na kuteleza amiin. Pia Allah awape ujira mwema wote waliofanikisha Ujenzi wa ukuta wa kuzunguka eneo la makaburi amiin.

    ReplyDelete
  2. Naam, Mmungu awajaalie malazi mema jamii ya ndugu,wazee na wenzetu waliotangulia na kulala mahali hapo. Amin. Nilipata bahati kutembelea sehemu hizo kuwazuru wazee wetu, ila nilisikitishwa kuona jinsi hali ya usafi nje ya jengo na ndani pia. Haina maana kama mahali kama hapo hapafai kuwa na usafi. Taka nyingi nje, ndani, mbele ya zile nyumba zilozkabili mlango wa kuingilia. Tujaribu kufikiria vipi kuweka unadhifu mahali kama hapo. Inafika mtu kukanyaga vyovyote tu jinsi hali ilivyo. Tujikusanye na hata kuwa na michango kwa kila ataeweza kugharimia au watu kujitolea nguvu kuweka usafi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naam ndugu Hamdani, maneno yako ni swadakta kabisa. hata mimi nimeliona hilo zaidi katika hili gate la kuingilia kwa kweli hujaa maji mengi sana siku za mvua hata kupita huwa taabu kidogo, hivyo tujitahidi kupatengeneza pahali hapa muhimu ambapo wazee, walimu mashekhe zetu mbalimbali wamelala hapo. Mola awape nuru katika makaburi yao wote amiiin.

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.