Habari za Punde

Mradi mpya wa uhifadhi wa uvuvi SWIOfish

 MKURUGENZI Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akielezea hatua wanazopaswa kufanya wajumbe wa Kamati tendaji ya PECA, baada ya kuja kwa mradi mpya wa uhifadhi wa uvuvi SWIOfish, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAJUMBE wa Kamati tendaji wa PECA wakiwa katika kazi za vikundi, ili kuchagua siku ya kufanya utambuzi wa maeneo ya bahari yenye samaki wa matumbawe kwa ajili ya mradi wa SWIOfish, kwenye mkutano uliofanyika, ukumbi wa makonyo Wawi Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mtambuzi wa ardhi Pemba Mohamed Salim, akionyesha hati ya kukabidhi mashamba yaliotambuliwa kwa ajili ya kwenda kwa msajili, ili kisha aweze kutoa hati kwa wamiliki wa mashamba ambayo yameshatambuliwa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 MRATIBU wa mradi wa Usimamizi wa uvuvi kusini, magharibi ya bahari ya Hindi SWIOfish, Ramla Talib Omar akiwasilisha taarifa na malengo ya mradi huo kwa wajumbe wa kamati tendaji wa PECA, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa makonyo Wawi Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

WAJUMBE wa Kamati tendaji ya PECA, wakimsikiliza Afisa Mdhamini Wizara ya mifugo na uvuvi Pemba, Mayasa Hamad Ali, wakati akifungua mkutano wa kuwasilisha mradi wa usimamizi wa uvuvi SWIOfish, uliofanyika ukumbi wa mikutano Makonyo Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.