Habari za Punde

Ofisi ya Mufti yakutana na waandishi wa habari Pemba, yawataka kudumisha amani na utulivu

 WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari kisiwani Pemba, wakiwa katika kikao cha pamoja na watendaji wa Ofisi ya Mufti Zanzibar, juu ya kuwataka kuendeleza amani na Utulivu Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Pemba Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud, akifungua kikao cha Waandishi wa habari Pemba na watendaji wa ofisi ya Mufti Zanzibar, huko katika skuli ya Madungu sekondari, juu ya kuendelea kuilinda amani na utulivu Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Utawala ofisi ya Mufti Zanzibar Shekhe Othaman Mohamed Saleh akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Umuhimu wa kuitunza Amani nchini, kwa waandishi wa habari Pemba huko katika skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KATIBU wa Mufti wa Zanzibar Shekh Fadhili Suleiman Soraga, akizungumza na waandishi wa habari kisiwani Pemba, mara baada ya kuwasilisha mada yake huko katika skuli ya Madungu Sekondari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWANDISHI wa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Pemba, Hamadi Shapandu Mwinyi akichangia katika kikao cha waandishi wa habari na Ofisi ya Mufti Zanzibar, huko katika skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.