Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Atembelea Eneo la Ujenzi wa Gati ya Kisasa Mpiga Duru Maruhubi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallamwinyi Khamis baada ya kuwasili katika eneo la maruhubi ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari kuanzia Januari mwakani mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kushoto akipata maelezo ya ramani ya ujenzi kutoka kwa Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk katika ziara ya kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari Maruhubi mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kushoto akipata maelezo ya ramani ya ujenzi kutoka kwa Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk katika ziara ya kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari Maruhubi mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein  kushoto akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk. Juma Malik Akili wakati alipofanya ziara kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari Maruhubi mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiuliza jambo alipokuwa akipewa maelezo na Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (kushoto) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt.Juma Malik Akili (wa pili kulia)akifuatia Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (katikati) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.