Habari za Punde

Jumuiya ya Vijana wa Paunia wa zamani yaanzishwa

Na  Khadija  Khamis  -Maelezo     Zanzibar  

Waziri  wa Fedha Mhe, Omar Yussuf Mzee amesema kuanzishwa kwa Jumuiya ya vijana wa paunia wa zamani (Young Pioneer Veteran Association)  kutasaidia vijana kujikwamua na umasikini pamoja na kujiepusha  na madawa ya kulevya.

Alisema tunashuhudia vijana wengi wa Zanzibar wanaendelea kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo madawa ya kulevya na kupelekea  mmong’onyoko wa maadili .

Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo wakati alipokuwa akizindua Jumuiya mpya isiyokuwa  ya  kiserikali Young Pioneer Veteran  Association yenye  lengo la kuwasaidia vijana  wa Zanzibar kimaendeleo.

Waziri  Mzee amekemea  tabia ya vijana kutokuwa na maadili na kujiingiza katika vikundi viovu jambo ambalo linapelekea kuhatarisha maisha na kwenda kinyume na silka na utamaduni wa Zanzibar .

“Hii inaonesha utofauti mkubwa  uliopo wa malezi heshima na tamaduni  zilizokuwepo awali  zimetoweka  kwa kuvaa nguo zisizostahiki na kupenda maisha ya anasa wakati uwezo wao ni mdogo.”Alisema Waziri  Omari.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano wa pamoja ili wawe na uwadilivu katika kazi zao waepukane na tamaa.


Sambamba na hayo Waziri Omari alianzisha harambee ya papo kwa papo na kuweza kukusanya fedha ya zaidi ya Tshs millioni 3,834,500 za papo kwa papo na Tshs Millioni 5,850,000 za ahadi  jumla shilling millioni 9,724,500 zilichangiwa Jumuiya hiyo .

Hata hivyo Waziri huyo aliahidi kutoa Komputa mpya moja na Printa mpya moja na pesa taslimu Tshs milioni moja na laki tano pamoja na Tshs milioni moja kwa ajili ya mchango wa mkewe ili kuweza kuisaidia jumuiya hiyo .

Nae Katibu wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii Vijana,Wanawake na Watoto  Asha Ali Abdalla kwa niaba ya Waziri Uwezeshaji ,Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainabu Omar Muhammed alisema ushirikiano wa jumuiya utaleta mafanikio kwa vijana wa Zanzibar  na  Jumuiya wasisiste kuitumia wizara yake kwa matatizo mbali mbali ambayo  yatayojitokeza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.