Habari za Punde

Timu ya Mafunzo Kuagwa Rasmin Kuelekea Nchi Congo katika Mchezo Wake wa Marudio na Timu ya AS Vita

Kikosi cha Timu ya Mafunzo inayotarajiwa kuondoka hivi karibu  kuelekea Nchi Congo katika Mchezo wao wa Marudio na Timu ya AS Vita ya DRC, Katika Mchezo wao wa mwazo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Mafunzo imefungwa mabao 3--0.


Wawakilishi wa Zanzibar kwenye mashindano ya ligi ya klabu bingwa barani Afrika klabu ya Mafunzo inatarajiwa kuagwa rasmi kesho majira ya saa tano na nusu huko kwenye kambi yao Kilimani mjini Unguja.


Mkurugenzi wa ufundi wa Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar Masoud Attai alisema maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika na kikosi kitakabidhiwa bendera na mkuu wa wilaya ya mjini.Mbali ya kupoteza mchezo wao wa awali kwa kichapo cha bao tatu kwa bila kwenye dimba la Amaan lakini uongozi wa Mafunzo umedai utalipa kisasi hicho.Msemaji wa klabu hiyo Makame Fadau alisema morali ya wachezaji ipo juu kwani kila mmoja ameshajua makosa yake na kuyafanyia marekebisho.Mafunzo ilipokea kichapo hicho kutoka kwa wageni wao klabu ya AS Vita kutoka DR Congo ambayo ilikua imesheheni wanandinga saba waliokuwa kwenye timu ya taifa ya nchi hiyo katika mashindano ya CHAN kigali nchini Rwanda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.