Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakiangalia Majina yao katika Ubao uliobandikwa Majina ya Wapiga Kura wa Kituo hicho cha Skuli ya Sekondari Kitope Wilaya ya Kaskazini Unguja walipofika Kupiga kura katika Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakiwa katika foleni wakisubiri zamu ao kwa ajili ya Kupiga Kura ya Urais wa Zanzibar, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Udiwani wakiwa katika Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Sekondani Kitope Zanzibar.
Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) akihakiki jina la Mpiga Kura katika Daftari la Wapiga Kura mwananchi aliyefika Kituoni hapo kwa ajili ya kupiga Kura yake. Kumchagua Rais wa Zanzibar Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Diwani.
Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakiwa katika Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Sekondari Kitope Zanzibar wakisubiri zamu zao kupiga Kura katika Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar.
Mzee Mayala Muhangwa akisaidiwa na Mtoto wake Makelele, kutimiza haki yake ya Kidemokrasia ya Kupiga Kura kumchagua Kiongozi anayemtaka wakati wa zoezi la Uchaguzi wa Marudio Zanzibar, akiwa katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kitope Jimbo la Mahonda Zanzibar.
Mwananchi wa Jimbo la Mahonda Mayala Muhangwa akipiga Kura yake katika Kituo cha Wapiga Kura cha Skuli ya Kitope Zanzibar akisaidiwa na Mtotio wake Makelele.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mahonda Mhe Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wakati akiwasili katika Kituo cha Kupiga Kura cha Skuli ya Sekondari Kitope Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akielekea katika Kituo chake cha Kupigia Kura katika Skuli ya Sekondari Kitope Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika foleni kusubiri zamu yake ili aweze kupiga Kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Sekondari Kitope Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mahonda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisubiri kukabidhiwa karatasi za kura ili kutumia haki yake ya msingi ya kupiga Kura.
Balozi Seif akitoka katika Chumba maalum cha kumpigia Kura Kiongozi amtakaye katika kituo cha wapiga kura Skuli ya Sekondari Kitope Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi akipiga Kura yake katika Kituo cha Wapiga Kura cha Skuli Sekondari Kitope Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi akitoka Chumba cha Kupigia Kura katika Skuli ya Sekondari Kitope Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakimsikiliza Mgombea Wao wa Uwakilishi Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kitope Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika Zanzibar kuripoti habari za Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar uliofanyika leo March 20, 2016. Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiondoka katika eneo la kupigia kura katika Skuli ya Sekondari ya Kitope Wilaya ya Kaskazini Unguja. baada ya kupiga kura yake.
Mwananchi wa Jimbo la Mahonda akisubiri kukabidhiwa Karatasi za kupigia Kura kutoka kwa Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Mwananchi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar Akipiga Kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura katika Skuli ya Sekondari ya Kitope.
No comments:
Post a Comment