Habari za Punde

BREAKING NEWS: Dkt Shein atangaza Baraza lake la Mawaziri

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza jipya Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo la Mapinduzi kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7 na taasisi za wizara alizozivunja amezihamishia ambapo  katika baadhi ya wizara za sasa.

Mawaziri hao watawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
      Mhe. Issa Haji Ussi Gavu.

2). Wizara nchi Afisi ya Rais Katiba  Sheria Utumishi wa Umma na utawala bora – 
     Mhe. Haroun Ali Sleiman.

    Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Katiba .Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora 
      Mhe. Khamis Juma Maalim.  

3). Wizara ya nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ 
      Mhe. Haji Omari Kheir.

4). Wizara ya nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa  Rais 
      Mhe. Mohammed  Aboud. Mohammed


5). Waziri wa Fedha na Mipango 
      Mhe. Dk. Khalid Salum Mohd.

6). Wizara ya Afya
      Mhe Mahmoud Thabit Kombo.

Naibu Wizara ya Afya .
      Mhe.Harusi Said Suleiman.

7). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
      Mhe.Riziki Pembe Juma 

Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali.
      Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri.

8). Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
      Mhe. Balozi Amina Salum Ali.

9). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji
     Mhe Balozi Ali Karume 

Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji 
Mhe.Mohamed Ahmed Salum.

10). Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo 
         Mhe.Rashid Ali Juma 

Naibu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo.
          Mhe.Chumu Kombo Khamis.

11).Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi
        Mhe.Hamad Rashid Mohd 

Naibu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi.
   Mhe.Lulu Msham Juma.

12).Wizara ya  Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
        Mhe.Mauldine Castiko.

13). Wizara ya Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
       Mhe.Salama Aboud Talib.

 Niabu Waziri Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
       Mhe.Juma Makungu Juma.

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, amewateuwa wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri wasio kuwa na Wizara Maalum 

Mhe Said Soud Said - Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe Juma Ali Khatib -Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum. 
Uteuzi huo umeaza leo tarehe 9/4/2016.

 Waheshimiwa wanatarajiwa kuapishwa kesho Ikulu jumapili 10April 2016,Saa 3 asubuhi kwa ajili ya kuapishwa. Ikulu Zanzibar   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.