Habari za Punde

Dk Shein awaapisha viongozi wa Taasisi mbali mbali Ikulu leo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla  kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
 Washauri wa Rais wa Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali Serikali ya Mapinduzi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]  
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa   Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Raya Issa Msellem  kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]

 Baadhi ya Viongozi mbali mbali Serikali na wananchi waliohuria katika hafla ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw, Mzee Ali Haji  kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Mwanahija Almasi Ali  kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
 Baadhi ya Viongozi mbali mbali Serikali na Wananchi waliohudhuria katika hafla ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi walipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Alo MOhamed Shein,[Picha na Ikulu.]  
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                              30.4.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha viongozi mbali mbali kushika nyadhifa katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Walioapishwa ni Salmin Amour Abdallah kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Asaa Ahmad Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Raya Issa Msellem kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mzee Ali Haji kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwanahija Almasi Ali kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Hafla ya kuwaapisha viongozi hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Miongoni mwao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman, Waziri wa Fedha na Mipango Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.