Habari za Punde

Jinsi gani Zanzibar huibiwa mapato kutoka kwenye sekta ya utalii

Ok!! This is how it works.
Kwa mfano muitaliano anajenga hoteli kubwa Zanzibar mathalan eneo la Nungwi. Wakati huo huo anafungua kampuni nyingine pale Panama au Isles of Man yenye undugu na hoteli yake iliyoko Zanzibar. Amefungua Panama kwa sababu kodi hakuna au ipo kiduchu sana. 

Watalii au wateja wake asilimia kubwa wanatoka Ulaya, wata book hoteli ya Zanzibar kupitia kampuni tanzu iliyoko Panama kwa $800 per night ( kwa usiku mmoja) mathalan.

 Wateja wakiwa wengi anawachukulia charter flight wanapelekwa Zanzibar moja kwa moja. 

Sasa wale wateja au watalii wakisha tumia hoteli wanaenda zao makwao, huku nyuma hoteli iliyoko Zanzibar ina raise invoice na kuipelekea kampuni yake tanzu iliyoko Panama kutaka kulipwa. 

Hiyo invoice itasomeka kuwa hawa watalii au wateja walikuwa wakichajiwa $100 per night na si $800 per night kama walivyolipa kwenye kampuni tanzu iliyoko Panama. 

Kwa maana hiyo hoteli ya Zanzibar kwenye financial report zake itaripoti mauzo yenye pungufu ya $700 per night kwa kila kichwa cha mteja au mtalii. 

Automatically mauzo yatakuwa pungufu sana by $700 na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar - SMZ kupitia ZRB Zanzibar Revenue Board ama TRA wataishia kupata corporate tax ndogo sana, tu kwasababu mauzo yamepunguzwa sana kiasi cha $700 per night kwa kila kichwa. 

Kwa maelezo yangu hapo unaweza ona ni jinsi gani ilivyo ngumu kwa SMZ kunufaika na rasimali yake ya utalii. Hii inatumika na takribani mahoteli yote kule Zenj hata kwenye mbuga za bara.
Hizo hoteli hazitaishia hapo zitaanzisha foundations za kawaida ili kusaidia wakaazi huku wakionyesha fedha zile zimepekwa kwenye foundations wakati hata hazifiki na wanakuwa tayari wamepunguza kiwango cha kodi zaidi kwa sababu faida itazidi kwenda chini. 

Next time nitaongelea juu namna gani zao la samaki linavyochukuliwa poa na jinsi ambavyo likichukuliwa serious Zanzibar itapaa, ukiachana na mafuta na gesi zilizoko kisiwani humo. 

Sioni sababu ya msingi sana kwanini hiki kisiwa kiwe kama kilivyo sasa, naamini wangekuwa mbali sana hawa ndugu zetu. Solutions za hii kitu zipo.


kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Gabriel Mwang'onda

4 comments:

 1. zanziba kuna viongozi mzigo ndio tatizo

  ReplyDelete
 2. Mwandishi acha uchochezi, Z'bar hakuna matatizo ya aina hiyo na kama yapo tungekwisha yaona.

  Taarifa za serikali kupitia vyombo vya khabari( gazeti la mawio na ZBC) zinaonesha mapato ya utalii yanazidi kupanda siku hadi hadi siku!

  Na ni kwasababu hiyo Z'bar tunajivunia utalii wetu na ukuaji wa uchumi, pamoja na udogo wetu kijografia na uchache wa rasilimali naamini tunaweza kujitegemea bila ya msaada wa mtu yeyote!

  ReplyDelete
 3. Assalamu Alaykum!! Maalim nenda kuangalia vivutio vya watalii kama Betilajaibu hali yake na people palace hali iliyoko! Kupaka rangi wameshindwa licha kufanyia repair!! Au mnasuburi Against khan awapakie rangi! Bustani ya Forodhani inafaa kuwa malishio ya ngo'mbe kwa majani

  ReplyDelete
 4. Acha hayo magofu yabaki hivyo hivyo, hata yakiporomoka, kwanza hayo yalikua ni majumba ya wamanga ambao walitufanya watumwa!

  Hivyo unafikiri SMZ hawayaoni? wanayaona lakini wakifikiri madhila waliyoyapata wakulima na wakwezi wa visiwa hivi wanashinda inawauma!...kuyahudumia ni kutikuza usultani wa kiarabu!

  Wakitaka hao watalii waje, wasipotaka basi, kama alivyosema raisi wetu mmpendwa wakati wa kuapishwa " Zanzibar inajiuza yenyewe kwa jina lake"

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.