AFISA Mdhamini wizara ya nchi afisi ya
Makamu wa pili wa rais Pemba (katikati), Issa Juma Ali akisalimiana na
Mkurugenzi wa Uratibu kutoka TASAF makao makuu, Alphonce Kyriga, wakati
mdhamini huyo akiwasili kwenye ukumbi wa TASAF Pemba, kwenye mafunzo ya
wakufunzi wa maeneo ya mradi juu ya uundaji na utoaji mafunzo kwa kaya masikini,
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
MRATIBU wa mafunzo ya wakufunzi wa maeneo ya mradi, juu
ya uudaji na utoaji mafunzo kwa kaya masikini, Catherine Kisanga, akielezea
jinsi TASAF ilivyojipanga katika kukuza pato la walengwa, kwenye shehia na
vijiji kadhaa Tanzania, mafunzo hayo yalifanyika ukumbi wa TASAF Chakechake
Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAKUFUNZI wa maeneo ya mradi, juu ya uundaji
wa utoaji wa mafunzo ya vikundi vya kuweka akiba kisiwani Pemba, wakisikiliza
mada zinavyowasilishwa, kwenye mafunzo ya siku tano yaliofanyika ukumbi wa
TASAF Chakechake Pemba, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
MSAIDIZI wa Makamu wa pili wa rais Pemba Amran Massoud Amran akitoa neno la shukuran, kwenye mafunzo ya uundaji wa utoaji wa mafunzo ya vikundi vya kuweka akiba, kwa wakufunzi wa Kisiwani Pemba, mafunzo yaliofanyika afisi ya TASAF Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
PICHA ya pamoja ya watendaji wa TASAF makao makuu Tanzania bara na kisiwani Pemba, pamoja na wakufunzi wa mafunzo ya vikundi vya kuweka akiba kwa wale waliokwenye mpango wa kunusuru kaya maskini kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MRATIBU wa TASAF Pemba Mussa Said Kisenge
akichangia jambo kwenye mafunzo ya wakufunzi ya vikundi vya kuweka akiba kwa
wale waliokwenye mapango wa kunusuru kaya masikini, mafunzo yaliofanyika TASAF
Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
No comments:
Post a Comment