Habari za Punde

Taswira Wakati wa Hafla ya Kuapishwa Mawaziri Wapya Katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo Asubuhi.

Mawaziri Wateule wa Baraza la Mapinduzi la Mawaziri wa Zanzibar wakipitia hati zao za kiapo kabla ya kuaza kwa zoezi hilo lililofanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri Wapya.
Waheshimiwa  Mawaziri Wateule wasio kuwa na Wazira Maalum wakisubiri kula kiapo wa kwanza Mhe Siad Soud Said wa Chama cha AFP na Mhe Juma Ali Khatib wa Chama cha ADA-TADEA wakisubiri kula kiapo leo asubuhi.
Wanafamilia wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika viwanja vya Ikulu wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri. 
Viongozi wa Serikali na Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakishiriki katika hafla ya kuapishwa Mawaziri katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Mawaziri Wateule wakisubiri zoezi la kula kiapo katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri Zanzibar katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Wageni waalikwa wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri hafla iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.