Habari za Punde

Huawei kuzindua Y6 Pro kinara wa-siku nzima Tanzania Hatimae simu idumuyo na Charge mara dufu Tanzania! Huawei yaleta Y6 Pro Huawei yazindua simu ya kipekee Y6 Pro Nchini Tanzania


Shangwe haimaliziki: Kwa 

maneno mengine, haipendezi 

kukatisha furaha yako au 

Shangwe yako ghafla. Wakiwa 

na wazo hili kichwani, Kampuni ya simu Nchini Tanzania Huawei wamezindua simu mpya Y6 Pro. Ikiwa ni miongoni wa simu chache sokoni zenye uwezo wa kudumu na charge baada ya matumizi mengi, na hivyo kuruhusu Shangwe kudumu Zaidi.
Dar Es Salaam, Mei 2016; Huawei Tanzania leo wametangaza 
ujio wa Huawei Y6 Pro katika soko la Tanzania. Ongezo jipya 
katika familia ya simu za Huawei Y, ni la kipekee na ubora Zaidi 
lililoambatanisha hali ya juu ufanisi na utendaji kazi. Simu hii ni rafiki bora wa kuwa na wewe siku nzima hivyo kumwezesha mtumiaji kupata Zaidi katika simu yake ya mkononi.

Uzinduzi huu unakuja kwa wakati kuungana na Bodi ya mamlaka 

ya mawasiliano TCRA kuhimiza wateja kutumia simu zilizosahihi 

ama orijino na kudhibiti soko la simu bandia. Kuungana na 

Mpango wa TCRA, Huawei Tanzania wamepanga bei ya Y6 Pro 

iwe inayoweza kununulika na waTanzania wote, ili waweze 

kufaidi simu zilizo za ubora kwa bei nafuu. Huawei Tanzania wamejijengea heshima na jina kwa kukabiliana na matarajio katika soko la simu si duniani tu bali Tanzania.
“Mlolongo wa Y6 ni sahihi na mahususi kwa soko la Tanzania 

ambako, bei na matumizi yana umuhimu sawa. Simu hii ni 

mahususi kwa wale wanaopenda simu zao kukaa muda mrefu bila 

kuchaji. Ni simu pekee iliyo katika bei hii yenye uwezo wa 

kuhimili matumizi makubwa kwa siku kadhaa” alisema Bwana 

Huziangyang Jacko, Meneja Mkazi wa Huawei Tanzania.


Y6 Pro imetumia muundo wa kipekee na ubora wa hali ya juu. 

Zaidi ya smartphone, Y6 Pro inaleta uwiano katika urahisi, 

utumiaji na uzuri. Y6 Pro inawakilisha muundo wa maisha wa kuwa tayari muda wowote, hisia za ujana na mtazamo chanya ambao unawakilisha wateja wa Tanzania. Muundo wa simu hii ambao ni mzuri, wa kuvutia wenye muuonekano wa kipekee unaoruhusu watumiaji kushika simu kwa urahisi. Ikiwa ni sehemu ya muundo wao, wabunifu wa Huawei walifanya utafiti wa vifaa vilivyo vya ubora wa hali ya juu, muundo pamoja na mikunjo kwa ajili ya ukaaji ulio bora kiganjani.
“Tukiwa na shauku yetu katika teknolojia na uvumbuzi,
tumepangakuunda vitu vipya katika simu zetu. Tumepanga kuongeza vifaa makini ambavyo vitaboresha matumizi kwa siku nzima. Y6 Pro ni simu mahususi kwa watumiaji wenye matumizi mengi sana katika simu” alisema Bwana Huziangyang Jacko, Meneja Mkazi wa simu za Huawei.

Ikiwa na kamera ya mbele yenye mega pixeli 5 na nyuzi 84 

kwenyelensi yenye uwezo wa kutambua sura hivyo kufanya kujipiga picha kuwa rahisi na furaha zaidi. Ikiwezeshwa kwa ajili ya mwanga mdogo, Y6 Pro ina kamera ya nyuma yenye megapikseli 13 ambayo inauwezo wa kupiga picha usiku na mchana.

Smartphones zimeshika kasi ya kuwa kivutio kikuu nchini 

Tanzania, na Huawei Tanzania wanafanya kufurahia simu yako ya 

mkononi kwa wepesi zaidi. Muundo wa kipekee wa sauti wa Y6 

Pro unaongeza sauti kwa asilimia 150 na kusaidia sauti 

kutozuiliwa hata spika ya simu ikiwa imefunikwa. Pia watumiaji wanaweza ongea na kupiga simu hata katika mazingira yenye kelele nyingi.

Kwa Muonekano wa kipekee Y6 Pro zinapatikana nchini Tanzania 

katika miundo ya kipekee, ikiwa katika rangi nyeupe, kijivu na 

dhahabu. Muonekano wa Y6 Pro ni nyembamba na nyepesi 

kubeba.

Y6 Pro inajumuisha uwezo wa betri unaohitajika. Simu hii 

inajumuisha utumiaji mzuri wa betri unaoruhusu kutumia simu 

kwa zaidi ya masaa 90. Pia ina miundo kadhaa ya kuruhusu kuhifadhi chaji. Y6 Pro ina uwezo kutambua ikiwa inatumika au la hivyo kuiruhusu kuhifadhi chaji ikiwa haina matumizi. Y6 Pro ina uhakika wa kukaa na nguvu muda mrefu zaidi.

Y6 Pro imeundwa kuendana na mazingira yako ukiwa nyumbani, 

kazini au katika mizunguko. Huawei Tanzania inatazamia Y6 Pro 

kuwa simu ambayo inaendana na wa Tanzania na kutoa msaada 

katika matumizi yao.

Simu hii ina kuletea muundo wa kipekee na ubora wa hali ya juu 

ikiwa na mwonekano bora na kukupa furaha katika matumizi.

Katika kuelewa mahitaji ya watumiaji simu za smartphone 

Tanzania, Y6 Pro imeundwa na mfumo wa android wa 4G wenye 

hali ya juu ya ubora na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa 

wakati mmoja.

“Huawei ni moja kati ya wasambazaji wachache wa vifaa ambao 

wana maabara iliyohakikiwa ulimwenguni yenye vifaa vilivyobora 

zaidi. Tumeunda vifaa hivi kuhakikisha kuwa vinakidhi matarajio 

ya watumiaji, simu ambayo haitawaangusha na itadumu kwa muda 

mrefu zaidi,” alimalizia Bwana Huziangyang Jacko, Meneja Mkazi 

wa Huawei Tanzania.

Kuongeza usalama wa simu na kutambau simu zisizo halisi nchini, 

Huawei Tanzania imepanga kuleta simu zaidi na vifaa zaidi vvenye 

ubora na vilivo halisi, ili watanzania wote waweze pata kiurahisi 

simu zilizohalisi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.