Habari za Punde

Wananchi wa Jimbo la Mtopepo Zanzibar Wafanya Usafi wa Mazingira Mbeli ya Skuli yas Mtopepo Wilaya ya Magharibi A. Unguja.

Wananchi wa Jimbo la Mtopepo Zanzibar wakifanya Usafi wa Mazingira katika maeneo ya Jimbo lao, wakifanya usafi kando ya barabara ya Mkapa Zanzibar. 
Nao Vijana wa Jimbo hilo nao wamejitokeza katika zoezi hilo la usafi katika Jimbo lao.
Wananchi wa Jimbo la Mtopepo wakifanya usafi katika eneo la mbele la Skuli ya Mtopepo kwa kuzoa taka zilizolundikana katika eneo hilo.
Wananchi wakiwa katika zoezi hilo la usafi wa mazingira.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo yamefanyiwa usafi na sehemu ya eneo la mbele ya Skuli ya Mtopepo Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar akishiriki vilivyo katika zoezi hilo la usafi kwa kuzoa takataka katika eneo la skuli ya mtopepo Zanzibar.
Wananchi wakiendelea na zoezi hilo la usafi wa mazingira 
Waziri wa Afya Zanzibar akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtopepo Zanzibar wakati wa hafla ya zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya jimbo hilo.
Wananchi wa Jimbo la Mtopepo Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabi Kombo akizungumza na Waananchi hao wakati wa zoezi la kufanya Usafi katika maeneo yao ya makaazi na eneo la Skuli ya Mtopepo Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Mtopepo wakishiriki katika zoezi hilo la usafi wa mazingira katika eneo la skuli yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.