Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Waheshimiwa wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza wakiendelea na mkutano huo wa Bajeti. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, akihairisha Mkutano wa Baraza kwa mapunziko ya mchana kwa Wajumbe wa Baraza baada ya Kikao cha asubuhi cha maswali na majibu. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akitoka katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza baada ya kuahirisha Mkutano huo kwa mapumziko ya mchana.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifurahia jambo wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa wa kwanza Mhe Ali Juma Khatib, Mhe Balozi Ali Karume na Mhe Mwanaasha Khamis Juma. 
Mhe Balozi Ali Karume akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Zanzibar Mhe Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Said Hassan Said akizungumza na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Mgeni Hassan Juma.
Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Zanzibar Mhe. Ali Suleiman Ali (Shihata) akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said. wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano leo asubuhi. 
Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe Salama About Talib, akizungumza na Watendaji wa Wizara yake nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kipindi cha maswali na majibu  , 
Mwakilishi wa Jimbo la Paje Mhe Jaki Hashim Ayoub, akiwa makini akimsikiliza Mwakilishin wa Jimbo la Chumbuni Mhe. Miraj Khamis Mussa. wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana na sala.  

Waziri Asiye Kuwa na Wizara Maalum Mhe Juma Ali Khati, Uteuzi wa Rais, akisalimiana na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba Tanzania Ndg Haidar Madoweya. wakiwa nje ya jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakitoka katika Jengo la Baraza Baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa asubuhi kuchangia na kujibu maswali ya Wajumbe na kukamilisha kwa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Baraza,baada yaaliyechaguliwa mwazo nafasi hiyi Mhe Riziki Pembe kuchagulia Waziri wa Elimu, na Uchaguzi wa Pili ni wa Wajumbe wa Tume ya Bajeti ya Baraza, waliochaguliwa mwanzio Mhe Lulu Msham na Rashid Ali Juma.. Kwanafasi ya Wajumbe wa Tume ya Bajeti ya Baraza waliochagulia Mhe Mihayo Juma N'hunga. na Nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza amechaguliwMhe Mwanaasha Khamis Juma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.