Habari za Punde

Ligi Kuu Sita Bora Daraja la Kwanza Kati ya Mundu na White Bird. Timu Mundu imeshinda mchezo huo kwa Bao 1--0.

Wapenzi wa mchezo wa mpira wa miguu Zanzibar wakiwa nje ya Uwanja wa Amaan wakisubiri kuingia Uwanja kuangalia mchezo wa mwisho wa Ligi ya Sita Bora Ligi Daraja la Kwanza kati ya Mundu na White Bird. Katika mchezo huo Timu ya Mundu imeshinda bao 1--0 na kuungana na Timu za Chwaka, Taifa ya Jangombe, katika kupanda Ligi Kuu ya Zanzibar.  
Mashabiki wa Timu za Mundu na WhiteBird wakisuburi kuingia uwanjani kuangalia mchezo huo wa mwisho wa Ligi ya Sita Bora.
Wapenzi wakikata tiketi kuangalia mchezo huo wa mwisho wa Ligi ya Sita Bora uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.