Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar Balozi Seif Akagua Ujenzi wa Jengo la Skuli ya Mahonda leo.

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Walimu wa Skuli ya Msingi Kinduni alipofanya ziara na Timu yake kuangalia changamoto zinazoikabili Skuli hiyo
.
Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya usafi kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kinduni Bibi Miza Omar Mohammed kwa ajili ya utunzaji nwa mazingira kwenye skuli hiyo.
Muonekano wa Jengo Jipya la Skuli ya Msingi ya Kinduni linalojengwa  kwa nguvu za  wananchi wenyewe ili kupunguza msongamano wa wanafunzi skulini hapo.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif na Timu yake akikagua maendeleo ya matengenezo makubwa ya jengo la Skuli ya Msingi Mahonda aliloliwezesha kufanyiwa marekebisho hayo.
Balozi Seif akiwapongeza mafunzi wa matengenezo ya  jengo hilo kwa hatua kubwa waliyofikia katika marekebisho hayo yatakayotoa nafasi kwa wanafunzi kusoma bila ya wasi wasi.
 Balozi Seif akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa Katibu wa CCM Tawi la Kinduni Nd.Shaaban Moh’d Iddi ili viongeze kasi ya kukamilisha Matengenezo ya Tawi hilo.
Anayeshuhudia upande wa kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Hilika Ibrahim Khamis.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi la Kinduni Nd. Ali Ameir Khamis akimpatia maelezo Balozi Seif hatua iliyofikia ya matengenezo ya Ofisi ya CCM Tawi la Kinduni.leo 30/5/2016
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.