Habari za Punde

Acra Kuidhamini ZIFF


Katika maamuzi mazuri ya mwaka kiutamaduni ni uamuzi wa Acra kuidhamini ZIFF katika kuendesha jukwaa moja la ZIFF wakati wa Tamasha mwaka huu. Jukwaa hilo inaloitwa  Maswala Nyeti linatoa nafasi kwa wananchi kuzungumzia maswala yanayohusisha jamii moja kwa moja na kutoa nafasi ya sauti ya jamii kusikika.
Mwaka huu Swala Nyeti litakalozungumziwa ni kuhusu uwezekano wa Mji Mkongwe kuondolewa hadhi ya Urithi wa  Kimataifa na sababu zake.

Acra inatambua nafasi ya taasisi kama ZIFF katika kuongeza kasi ya maendeleo kwa jamii na ingependa kuisaidia katika kazi hiyo”, amesema Bi Laura Bassini, Meneja Mradi wa Acra.


Makubaliano hayo yaliyotiwa saini jana yanahusu utekelezaji wa miradi kadha wakati wa Tamasha la nchi za Jahazi litakalolaanza tarehe 9 Julai, mara baada ya Ramadhani.
Acra inadhamini miradi mitatu wakati huo ikiwa ni pamoja na:

1.     Kazi za maonesho ya wasanii mitaani ambayo itasimamiwa na Taasisi ya Nafasi kutoka Dar es salaam.
2.     Warsha ya “Urithi wangu” itakayoendeshwa na UQ Produzioni ya talia
3.     Jukwaa la Maswala Nyeti litakalozungumzia hilo swala la hatari ya Mji Mkongwe kuvuliwa taji la kuwa Urithi wa Kimataifa.
Fondazione Acra ni taasisi isiyo ya kiserikali inayofanya kazi kuhimiza kuondoa umasikini kwa kuleta maendeleo endelevu katika jamii mbalimbali duniani. Tasisis hiyo imeshatekeleza mamia ya miradi duniani.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba, ambapo Acra itatoa zaidi ya shilingi milioni kumi  Mkurugenzi wa ZIFF Profesa Martin Mhando alisema kuwa  pamoja na kazi ambazo ZIFF imekuwa inasimamia ni pamoja na kuongeza uwelewa kuhusu umuhimu wa taarifa katika jamii.
“Uelewa ni muhimu kama tunataka kitu kiwe endelevu na kwa kutambuwa umuhimu wa urithi wa kimataifa uliopo Mji Mongwe Acra inapenda kuchangia katika majukwumu hayo ya jamii hasa katika shughuli za kiuchumi.”Alisema Bi Bassini.
Watu wengi wana hamu ya kutoa mawazo yao kuhusu nafasi ya jamii katika swala hilo hivyo hata wadau kama UNESCO nao wamesema watakuwepo katika mazungumzoa hayo yatakayofanyika Ngome Kongwe usiku wa tarehe 13 Julai. Mazungumzo hayo yataonesha moja kwa moja na ZBC.
“Tunalisimamisha tamasha siku hiyo ili kuwapa wananchi nafasi ya kutoa mawazo yao maana ni haki yao ya kibinaadamu, kama ilivyoainishwa katika Umoja wa Kimataifa. Alimalizia Profesa Mhando
Umoja wa Kimataifa unashiriki katika ZIFF kupitia mashirika yake kama UNESCO, UNICEF na UNFPA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.