- Kuendesha
mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha kwa wanawake 2000.
Katika jitihada za kukuza ujasiriamali pamoja na kuongeza uwezo wa wanawake katika kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi, kampuni inayoongoza
visiwani Zanzibar, Zantel, leo imetoa kiasi cha shillingi millioni 10 kwa Jumuiya
ya Wakulima wa mwani Zanzibar
Kampuni ya Zantel pia
itaandaa mafunzo ya ujasiriamali,
utawala na usimamizi kwenye maswala ya fedha
kwa zaidi
ya wanawake 2000 yatakayoendeshwa katika kipindi cha
mwaka 2016 na
2017.
Akizungumza wakati wa hafla
ya makabidhiano hayo, Afsa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zantel, Bwana Benoit
Janin
alisema msaada wa Zantel kwa Jumuiya ya Wakulima wa
mwani Zanzibar unaendelea kuonyesha jitihada za
kampuni
ya Zantel katika kutekeleza ahadi zake kwa ajili ya ustawi
wa jamii ya
wanawake.
‘Wanawake wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali
ikiwemo tatizo la upatikanaji wa rasilimali,maarifa na
huduma, hivyo basi ili kukabiliana na changamoto hizi
tunaamini msaada utabadilisha
maisha ya wanawake wengi
wanaotegemea mradi huu katika kuendesha maisha’
alisema Bw.Janin.
Kilimo cha mwani ni shughuli
muhimu ya kiuchumi
inayotegemewa na wakazi wanaoishi katika miamba ya
matumbawe
ya visiwa vya Unguja na Pemba. Aina hii ya
kilimo inafanywa zaidi na wanawake
kwani kati ya wakulima
23,654 asilimia 80% ni wanawake.
'Imani yetu kama Zantel ni
kuwa uwezeshaji wa wanawake
ni jambo muhimu na sahihi la kufanya, kwa sababu mwanamke
ndiye nguzo ya jamii na hivyo tukitoa fursa za kiuchumi kwa wanawake tutaigusa
jamii pana zaidi’ alisema Bi Rachel Samren, Mwenyekiti wa Bodi wa Zantel na
Makamu wa Rais wa Mambo ya nje wa Millicom.
Akitoa shukurani zake za kwa
kampuni ya Zantel,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima wa mwani Zanzibar, Bi Pavu Mcha Khamis alisema msaada
waliopewa na kampuni ya Zantel utasaidia kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya
kilimo kama kamba kwa ajili ya kilimo cha mwani.
'Kwa kipindi kirefu tumekuwa
tunakabiliwa na changamoto
mbalimbali, hivyo tunaishukuru kampuni ya Zantel kwa
kutusaidia kuongeza upatikanaji wa vifaa vya kilimo pamoja
na fursa za masoko hivyo
kuwaongezea wanachama wetu
kipato’ alisema Bi Pavu Mcha Khamis.
Jumuiya ya Wakulima wa mwani Zanzibar ilianzishwa
mnamo mwaka 2010,kwa lengo la kuwaunganisha wakulima
wote wa zao la mwani
Zanzibar ili kuwawezesha kupata
muongozo wa kukuza na kuendesha kilimo bora cha
mwani
kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kupanua soko la zao
hilo.
No comments:
Post a Comment