Habari za Punde

Watendaji ZLSC Pemba wafanya ziara ya kubadilishana uzoefu wa kikazi

Watendaji wa Kituo cha Huduma za za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakiambatana mwendesha mashitaka, hakimu na mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi, wakipandisha ngazi za kituo cha Polisi Mkoani, tayari kwa ziara ya kubadilishana uzoefu wa kikazi
Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed, akifungua mkutano wa kubadilisha uzoefu wa kikazi, kwa watendaji wa Jeshi la Polisi, kutoka Mkoani na Mtambile, mkutano huo uliofanyika Mkoani
Mratibu Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akizungumza, kwenye mkutano wa kubadilisha uzoefu wa kikazi, kwa watendaji wa Jeshi la Polisi, kutoka kituo cha polisi Mkoani na Mtambile, mkutano uliofanyika Mkoani
Hakimu wa Mahakama wa Mkoa Chakechake, Khamis Simai, akifafanua jambo kwenye mkutano wa kubadilisha uzoefu wa kikazi, kwa watendaji wa Jeshi la Polisi wilaya ya Mkoani, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, afisi ya mkurugenzi wa mashitaka na Mamlaka ya kuzuia rushwa, mkutano uliofanyika Mkoani
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mkoani Hassan Khamis Juma, akitoa neno la shukuran, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kubadilisha uzoefu wa kikazi, kwa watendaji wa Jeshi la Polisi, Kituo cha Huduma za sheria, mahakama, afisi ya mkurugenzi wa mashitaka na Mamlaka ya kuzuia rushwa, mkutano uliofanyika kituo cha Polisi Mkoani Pemba
Watendaji wa Kituo cha Sheria wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, Mahakama, watendaji wa Jeshi la Polisi wilaya ya Mkoani, afisi ya mkurugenzi wa mashitaka na Mamlaka ya kuzuia rushwa, nje ya kituo cha Polisi Mkoani, mara baada ya mkutano wa pamoja na wa taasisi hizo, (Picha na Haji Nassor, Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.